BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA AKINGIWA KIFUA NA VIONGOZI WA AFRIKA, NI BAADA YA KUSHTAKIWA KATIKA MAHAKAMA YA JINAI YA KIMATAIFA YA ICC.


VIONGOZI wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya hatahudhuria kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC.

Katika azimio lao viongozi wa Afrika wamesema kuwa kiongozi yeyote wa taifa hatatakiwa kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani.

Viongozi hao wamefikia maazimio hayo baada ya kuishutumu ICC kuwa na kigeugeu – kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.

Mkutano huo umekusudia kuwatuma Marais watano wa Afrika nchini Uholanzi ili kuitaka Mahakama hiyo kuahirisha kesi ya rais Kenyatta itakayoanza November 12 ambapo pia mkutano huu umesema hata Naibu Rais William Ruto hafai kushtakiwa kwenye Mahakama hiyo ya ICC.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: