BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA RAIS JOSEPH KABILA YASITISHA MAZUNGUMZO NA KUNDI LA WAASI LA M23 NCHINI DRC.

The M23 rebel fighters walk down the hills to move to another positon near Sake in eastern Democratic Republic of CongoWaasi wa M23 wanaolalamikiwa kuvuruga amani ya Mashariki ya Kongo.

MAZUNGUMZO ya amani kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 yamesitishwa tena licha ya Umoja wa Mataifa kuweka msuk
umo wa kuendelea kwa majadiliano ya pande hizo mbili.

Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea mjini Kampala Uganda tangu Septemba mwaka huu ambapo kila upande umetoa tamko lake kuhusiana na kusitishwa kwa mazungumzo hayo.

Msemaji wa Serikali ya Kongo Lambert Mende amesema kuwa mazungumzo yamesitishwa kutokana na kutofikiwa makubaliano kuhusu msamaha kwa M23 na jinsi watakavyo jumuishwa katika jeshi la Taifa la nchi hiyo FARDC.

Mjumbe wa M23 katika mazungumzo hayo Roger Lumbala alisema kumekuwa na vikwazo lakini wao wako tayari kurejea kwenye meza ya majadiliano wakati wowote.

Awali serikali ilionya kuwa majadiliano yaliyoanza upya mwezi Septemba chini ya shinikizo la Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu yalikuwa yanakwenda taratibu mno hali iliyoashiria mwisho wa maafikiano. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: