Wakulima wa Afrika Mashariki wahudhuria warsha juu ya namna ya kuimarisha mazao yao.
WIZARA ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania imezungumzia hatua
ya baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC za
Kenya, Uganda na Rwanda kufanya mikutano kati ya nchi tatu kujad
ili
masuala ya jumuiya hiyo pasipo kuzishirikisha nchi za Tanzania na
Burundi.
Tanzania kupitia wizara hiyo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema
kuwa pamoja na kuwa mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika
Mashariki EAC unaruhusu nchi wanachama kuwa na ubia, ni lazima suala
linaloenda kutekelezwa chini ya mfumo huo liwe limejadiliwa na
kukubalika na nchi zote wanachama.
Katika mikutano kati ya nchi tatu, Kenya, Uganda na Rwanda, uliofanyika
june 24 hadi 25 Entebbe Uganda, wajumbe walikubaliana juu ya mambo mbali
mbali ua miundo mbinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa
kutoka Mombasa kuelekea Kigali kupitia Kampala, ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia Uganda hadi Kenya na ujenzi wa
kiwanda cha kusafisha mafuta Uganda.
Zauidi ya hayo walijadili juu ya kuongeza namna ya kupata umeme zaidi,
kuanzisha mfumo moja wa forodha, kuharakisha Shirikisho la Kisiasa,
vitambulisho vya kitaifa kutumika kama hati ya kusafiria na visa ya
pamoja ya utalii.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Vedastina Justinian amewaambia waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam Jumatatu kwamba kufuatia hali hiyo, baraza la mawaziri la
Afrika Mashariki limemtaka Mwenyekiti wa baraza la mawaziri ambae ni
waziri wa mambo ya Kigeni wa Uganda kutoa taarifa ya kina kuhusu
mikutano iliyofanywa na athari zake kwenye utangamano wa Jumuiya ya
Afrika Masharki katika mkutano wa 28 wa baraza la mawqaziri unaotarajiwa
kufanyika Novemba mwaka huu mjini Arusha.
Hata hivyo Tanzania imesema ikiwa ni sehemu ya mtangamano huo wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, ina nia ya kuhakikisha inatekeleza
makubaliano ya pamoja kulingana na matakwa ya Mkataba wa kuanzishwa
jumuiya hiyo unaotaka kushirikisha pia wananchi katika kila hatua.
Tanzania katika mkutano wa 27 wa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki uliofanyika Arusha Agosti 31 mwaka huu ilitaka kujua hatma
ya mtangamano wa jumuiya ya afrika mashariki na kutaka ufafanuzi
kutokana na ukweli kwamba baadhi ya mambo ambayo nchi za Kenya, Uganda
na Rwanda zinayajadili na kuyatolea amaamuzi , bado majadiliano yake
yanaendelea katika ngazi ya jumuiya.
Mkutanano mwingine wa baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo ya afrika
mashariki ambako ndiko kutatolewa ufafanyzi huo unatarajiwa kufanyika
mwezi ujao.voaswahili.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment