TASWIRA YA VIONGOZI WA JUU WA SERIKALI KATIKA SIKUKUU YA EID EL HAJJ, JK NA MAKAMU DAR ES SALAAM, DK SHEIN NA MAALIF SEIF WASHEREHEKEA VISIWNI ZANZIBAR
Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu muda mfupi baada ya kushiriki Swala ya EID iliyofanyika katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro).
Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu muda mfupi baada ya kushiriki Swala ya EID.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Al-Farouk (Bakwata) Kinondoni kwa ajili ya swala ya Eid El-Haj kitaifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Uwanja wa Mpira Marumbi, paliposwaliwa Swala ya Idd el Hajj, kitaifa katika Kijiji hicho Wilaya ya Kati Unguja. (Picha na Ramadhan Othman).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kulia) akijumuika na Waislamu wengine katika Swala ya Idd el Hajj iliyoswalishwa na Sheikh Rashid Ali Vuai, (mbele).
Waislamu na wananchi wa jimbo la Chwaka wakisilikiza hotuba ya swala ya Idd el Hajj.iliyotolewa na Sheikh Sheikh Rashid Ali Vuai, ambapo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbakli wa Kitaifa (hawapo pichani).
Akina mama waliohudhuria katika Swala ya Idd el Hajj, wakisilikiza hutuba iliyokuwa ikitolewa na Sheikh Rashid Ali Vuai, mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na wazee na wananchi baada ya kuswali Swala ya Idd el Hajj, Kitaifa iliyoswliwa katika kijiji cha marumbi Uwanja wa Mpira, Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na mashehe katika ukumbi wa Hotel ya Coconut Tree, baada ya kuswali swala ya Idd el Hajj.
Viongozi mbalimbali na wananchi wakiwa katika sherehe za baraza la EId lililohutubiwa na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA), kampasi ya Tunguu Unguja.
Baadhi ya Akina Mama wliohudhuria katika Baraza la Eid El Hajj lililofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA, kampasi ya Tunguu.
Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akitoa hutuba yake kwa wananchi katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj, katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA leo.
Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya hutuba ya baraza la Idd El Hajj, iliyotolewa na Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein katika Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA).
Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akipokea salamu ya utii ya Kikosi cha Polisi FFU, baada ya kumalizika kwa Baraza la Idd el Hajj katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha SUZA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika swala ya sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria katika swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, katika Msikiti wa Anwaar.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, wakati akiondoka katika msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini wa dini ya kiislam.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini hao leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
0 comments:
Post a Comment