Maji ya Ndanda Springs pichani.
KIWANDA cha Maji cha Ndanda Springs kilichopo kijiji cha Mwena eneo
la Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara kimefungiwa kuzalisha maji hayo
kutok
ana na madai ya kushuka kwa ubora wake.
Ofisa Afya wa Mkoa wa Mtwara, Jamal Mbava alisema katika ukaguzi
uliofanywa Agosti, 12 na 13 mwaka huu wilaya ya Newala mkoani hapa
ulibaini uwepo wa takataka zinazoelea na kuonekana kwa macho katika
katoni 93 Mussa Kazibure.
Kwa mujibu wa barua ya ofisa huyo kwenda kwa mkurugenzi wa kiwanda
hicho ya tarehe 23/09/2013 yenye kumbukumbu Na: RHO/TFDA/5/63 maji hayo
kukutwa na takataka ndani ni kukiuka kifungu cha sheria Na 30 (2) cha
TFDA.
Alisema katoni hizo zikiwa na batch namba tofauti yaani 040912/160812
na 030912 zilikamatwa na kuwekwa katika ofisi ya afya ya wilaya hiyo
huku sampuli za maji hayo zikipelekwa kwa mamlaka ya Chakula, Dawa na
Vipodozi (TFDA) Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
“ Kwa mamlaka niliyonayo chini ya sheria za Tanzania No. 1 ya
chakula, dawana vipodozi ya mwaka 2003 kifungu cha 106 (F), nikaandika
na kutoa mari ya kufunga kiwanda hicho mkapa hapo tutakapopata majibu ya
kimaabara kutoka TFDA DSM” alisema Mbava.
Aliongeza kuwa “ Kwa taarifa hii ambayo naitoa kwenu naomba wananchi
kuchukua taadhari wakati wa kutumia maji hayo ya kunywa , popote pale
maji hayo yanapofika na pindi wakibaini hasa batch hizo na zinginezo
ambao chupa zake zitaonekana kuwa na taka zinazoelea ambazo kitaalamu
zinaitwa kwa ujumla kwa jina moja tu la ‘Impurities’ watoetaarifa katika
ofisi za afya zilizo karibu yao”. CHANZO http://kusini.wordpress.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / TFDA HAITAKI MCHEZO !!! CHAKIFUNGIA KIWANDA CHA MAJI CHA NDANDA SPRINGS KWA MADAI YA KUSHUKA KWA UBORA WAKE MKOANI MTWARA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment