BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUME YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA JUU YA UCHUNGUZI WA MATOKEO KIDATO CHA NNE YAIBUA MADUDU.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA KIGURUNYEMBE ILIYOPO MANISPAA YA MOROGORO WAKIFANYA MTIHANI WA TAIFA SOMO LA KISWAHILI SHULENI HAPO MWAKA 2012.  PICHA/MTANDA BLOGWaziri wa wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa.

DAR ES SALAAM. 
RIPOTI ya Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mapema mwaka huu, iliibua madudu mengi ambayo hayajaw
ekwa hadharani.
Wajumbe waliounda kamati hiyo kwa nyakati tofauti waliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa waligundua mambo mengi yanayodhihirisha udhaifu mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya elimu nchini.
Sehemu kubwa ya matokeo ya uchunguzi huo inasemekana yamejikita zaidi katika kuzitupia lawama taasisi za Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Udhaifu wa kiutendaji kati ya taasisi hizo mbili unadaiwa umechangia kwa wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani ya Kidato cha Nne mwaka jana kiasi cha kuilazimisha Serikali kuunda tume kuchunguza tatizo kutokana na kilio kikubwa cha wadau wa elimu na wananchi.
Viongozi watatu waandamizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hawakupatikana kuzungumzia uchunguzi huo jana.
Simu ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa haikupatikana kabisa pale ilipopigwa.
Naye Naibu wake, Philipo Mulugo alijitetea kwamba alikuwa na shughuli nyingi na hivyo hakuwa na muda wa kuzungumzia suala hilo wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome hakupokea kabisa simu yake.
Matokeo hayo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 walipata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakiwa wamepata daraja la nne. 

Katika mtihani huo, watahiniwa 397,136 walikuwa wa shule na 68,806 wa kujitegemea.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu Pinda aliamua kuunda tume iliyoanza kufanya kazi kuanzia Machi hadi Juni mwaka huu.
Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Profesa Mchome ilimkabidhi Waziri Mkuu ripoti Juni 15, mwaka huu.
Hata hivyo, ripoti hiyo haijawahi kutolewa hadharani baada ya tume kumaliza kazi yake.
Badala yake imeshuhudiwa Profesa Mchome, ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania akipandishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: