Msanii mkongwe katika anga ya
muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake kibao
waliofurika vilivyo ndani ya uwanja wa Majengo mjini Moshi ambapo
tamasha la Serengeti fiesta linafanyika.
Mwanadada Linah akimpagawisha
shabiki wake vilivyo jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la serengeti
fiesta 2013,kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Sehemu ya umati wa watu kutoka mjini Moshi wakiwa kwenye tamasha la fiesta usiku ndani ya uwnaja wa Majnego.
Mwanamuziki wa bongofleva kutoka THT,pichani kati Linah akicheza kwa madaha kabisa na madansa wake jukwaani usiku huu.
Mwanadada aliyewahi kufanya vyema kwenye shindano la BSS,aitwaye Menina akiimba jukwaani na madansa wake.
Wasanii wanaounda kundi la Jambo
Skwadi wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee kabisa usiku huu
kwenye tamasha la serengeti fiesta linalofanyika kwenye uwanja wa
Majengo mjini Moshi. MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
0 comments:
Post a Comment