BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WA HABARI SASA ROHO MKONONI.

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri. Neville Meena akizungumza mara baada ya waandishi wa habari kumaliza maadamano yao ya Amani kutoa ujumbe wao kwa jeshi la Polisi kutokana na kupot
eza maisha kwa  mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa katika vurugu kati ya Polisi na Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa hivi karibuni.


IRINGA.
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, amesema sekta ya habari kwa sasa ipo katika wakati mgumu na hatari kuliko wakati mwingine wowote huko.

Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mjini Iringa jana, alisema hatari hiyo inatokana na kutokuwepo kwa sheria bora za kusimamia usalama wa waandishi wa habari na watoa habari nchini.

Alisema pamoja na hali hiyo inayoibua mapambano baina ya wadau wa tasnia hiyo na Serikali wahariri na waandishi wa habari wana jukumu la kusimamia ukweli katika kutekeleza majukumu yao na kufanya kazi kwa weledi.

“Tasnia ya habari kwa sasa ipo katika kipindi kigumu na waandishi wapo katika hatari kuliko wakati mwingine wowote, njia pekee kujilinda na hali hiyo ni waandishi na wahariri kuandika habari za kweli na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu,”alisema Mukajanga.

Mukajanga aliwataka wahariri kuepuka kuingia kwenye mgawanyiko wa kutumikia makundi ya watu ama watu binasfi kwa maelezo kuwa kufanya hivyo na kujiingiza katika hatari zaidi.

“Epukeni kutumikia makundi ya watu fulani ama mtu binafsi, fanyeni kazi kwa kuzingatia weledi na maadili ya kazi zenu. ”alisema.

Alisema wahariri wanapaswa kuzingatia usalama wa waandishi wa vyombo vyao kwa kuzingatia na kuangalia uzuri na ubora wa habari wanazopokea. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: