Wanajeshi wa Kundi la Waasi la M23 wakiwa katika Mji wa Goma uliopo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC REUTERS/James Akena.
DAR ES SALAAM.
KUNA ripoti kwamba Kundi la Waasi la M23 ambalo limekuwa likisababisha mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), limesambaratishwa katika operesheni kali iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya vikosi vya nchi hiyo na vile vya Umoja wa Mataifa.
DAR ES SALAAM.
KUNA ripoti kwamba Kundi la Waasi la M23 ambalo limekuwa likisababisha mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), limesambaratishwa katika operesheni kali iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya vikosi vya nchi hiyo na vile vya Umoja wa Mataifa.
Taarifa za kusambaratishwa kwa kundi hilo zimekuja
siku chache baada ya kuzuka mapigano makali yaliyosababisha kuuawa kwa
askari mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni
Rajab Ahmed Mlima aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika operesheni
ya kuwaokoa raia, waliokuwa wamenasa kwenye eneo la mapigano.
Wanajeshi wa Tanzania ni sehemu ya vikosi vya
Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani huko Congo (Monusco) vyenye askari
pia kutoka Afrika Kusini na Malawi, vikiwa na kazi ya kupambana na
kupokonya silaha za vikundi vya waasi wanaopigana kwenye nchi hiyo.
Mkuu wa Vikosi vya Monusco, Martin Kobler
alithibitisha taarifa za kusambaratika kwa kundi hilo la M23 na kuongeza
kuwa vikosi vya Serikali na vile vya UN vilikuwa vikiendesha doria
katika maeneo yaliyokuwa yakidhibitiwa.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)
liliripoti jana kuwa Kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa amekimbia
mashambulizi kwa kuvuka mpaka na kuingia Uganda wakati majeshi ya Congo
yalipokuwa yanakaribia ngome yao.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa juzi, Kobler alisema Kundi la M23 limepoteza
mwelekeo.
“Ninachoweza kusema sasa tumefanikiwa
kuwasambaratisha waasi na sasa vikosi vyetu kwa kushirikiana na vile vya
DRC Congo vinadhibiti maeneo yote,” alisema Kobler.
Hata hivyo, Msemaji wa JWTZ, Meja Eric Komba
alisema asingeweza kutoa maelezo ya kina kuhusiana na taarifa za
kusambaratishwa kwa kundi hilo la waasi, kwa vile wazungumzaji wakuu wa
suala hilo ni Umoja wa Mataifa.
“Kama mnavyojua sisi tumekwenda DRC Congo kwa
ridhaa ya Umoja wa Mataifa, hivyo kufanikiwa ama kushindwa kwa
operesheni yoyote iko chini ya Umoja wa Mataifa wenyewe.
Tanzania haiwezi kusema kwamba vikosi vyetu vimewasambaratisha waasi wakati mwenye jukumu la mwisho kutoa tamko hilo ni UN wenyewe,” alisema Meja Komba.
Tanzania haiwezi kusema kwamba vikosi vyetu vimewasambaratisha waasi wakati mwenye jukumu la mwisho kutoa tamko hilo ni UN wenyewe,” alisema Meja Komba.
Wakati hali ikiripotiwa kuwa hivyo, taarifa
zinasema kuwa kundi hilo la M23 limemeguka mara mbili na kuzaliwa kundi
jingine linalojiita M18. Maofisa wa Serikali ya Uganda wamesema kuwa
kujitokeza kwa kundi hilo jipya kunaashiria kifo cha Kundi la M23 ambalo
kwa miaka mingi limekuwa likidhibiti maeneo yanayotajwa kuwa na utajiri
wa madini.
Kundi hilo la waasi ambalo limekuwa likidaiwa
kupata msaada wa kijeshi kutoka kwa mataifa ya Rwanda na Uganda,
limeelezwa kuelemewa nguvu na limesalimu amri katika maeneo liliyokuwa
likishikilia.
Vikosi hivyo vya M23 vilianzisha upya mapigano
hayo na kufanikiwa kuteka baadhi ya miji muhimu baada ya kuvunjika kwa
mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea Kampala, Uganda. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment