BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WABAKAJI WAMBAKA MSICHANA KISHA MKUTUPA KATIKA SHIMO LA CHOO NA KUVUNJIKA UTI WA MGONGO, WABAKAJI WAPEWA ADHABU YA KUFYEKA NYASI NA POLISI KISHA KUACHIWA HURU NCHINI KENYA.

Liz alibakwa na watu waliomtupa kwenye shimo la choo na kumvunja uti wa mgongo.

MAMIA ya waandamanaji nchini Kenya wamewasilisha polisi hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka msichana huyo wa miaka 16.
  
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume na kutupwa katika shimo la choo ambapo alivunjika mgongo wake.
Wanaume wanaotuhumiwa kumbaka msichana huyo waliamriwa na polisi kukata nyasi kama adhabu ya kitendo hicho.


Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.


Waandamanaji hao wameelezea kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili kumtendea haki msichana huyo.


Pia wanataka polisi waliowaadhibu washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.


Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.


Kampeini hii imekuja baada ya msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.


Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi. BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: