AGIZO
la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, la kuundwa kwa timu ya kusaka mwafaka wa
mgogoro baina ya Serikali na wadau wa usafirishaji ndani ya mwezi mmoja
bado limekw
ama.
Wasafirishaji ambao ni Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa) na Chama cha
Wamiliki wa Malori (Tatoa) waliogoma kwa siku kadhaa wakipinga serikali
kufuta msahama wa ongezeko la tozo ya asilimia tano katika mizani
kuanzia Oktoba 1, mwaka huu, hadi jana walisema hawajapata maelezo
yoyote kutoka serikali juu ya utekelezaji wa maagizo ya Pinda.
Mgomo huo ulitokana na tangazo la kufutwa kwa msamaha huo lilitolewa na
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na kusababisha malalamiko kutoka kwa
Tatoa na Taboa na baadaye kugoma.
Oktoba 10, mwaka huu, Waziri Pinda alitoa mwezi mmoja kwa Wizara ya
Ujenzi kukutana na wadau mbalimbali kwa kwa ajili ya kupitia hoja zote
zinzolalamikiwa na washafirishaji hao.
Pinda aliingilia kati ili kumaliza mgomo wa malori ambao ulikuwa umedumu
kwa zaidi ya wiki moja tangu kuanza kutekelezwa kwa amri ya Waziri
Magufuli.
Wadau hao ni Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taboa na
Tatoa.
Hata hivyo, hadi kufikia jana takribani wiki mbili baada ya agizo la
Pinda, hakuna kilichofanyika ikiwamo kuwajulisha wadau hao lini
wanatakiwa kuhudhuria vikao vya kusaka mwafaka.
Msemaji wa Tatoa, Elias Lukumay, akizungumza na NIPASHE kuhusu hatua
iliyofikiwa ya kuundwa kwa timu hiyo, alisema hadi sasa hawajapewa
taarifa yoyote ya kuitwa au maelekezo juu ya kuundwa kwa timu hiyo.
Alisema kwa upande wao wameshamwandaa mwakilishi atakayekwenda
kuwawakilisha katika vikao hivyo, lakini wanashangaa kuona siku
zinakwenda bila kupewa taarifa yoyote ya kuitwa.
“Toka siku ile Waziri Mkuu alipotoa lile agizo hadi leo (jana) hatujaona
barua wala wito wowote wa kutakiwa kuhudhuria katika timu ingawa sisi
tumeshajiandaa,” alisema Lukumay.
Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu, alipotafutwa alisema hawajapata
taarifa yoyote ya kuitwa katika timu hiyo na hawajui kinachoendelea.
Alisema Serikali inatakiwa kuwa makini katika jambo hilo bila
kulipuuzia kwa kuwa linaweza kuleta athari kubwa zaidi za kiuchumi.
Alisema Serikali haiwezi kufanya maendeleo yoyote katika sekta ya usafirishaji bila kuwashirikisha wadau wa usafirishaji.
Mrutu alisema ni jambo la kushangaza hadi sasa hakuna sera ya usafirishaji na serikali imekaa kimya bila kuchukua hatua zozote.
Ofisa Habari katika Waziri Mkuu, Augustin Tendwa, alipoulizwa hatua
iliyofikiwa katika uundwaji wa timu hiyo, alisema Ofisi ya Waziri Mkuu
inatakiwa kupokea taarifa ya kuundwa kwa timu hiyo kutoka katika Wizara
ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.
Alisema ni vigumu kufahamu kama mrejesho umepelekwa ofisini hapo kwa
kuwa Waziri Mkuu na wahusika wakuu wa kuyatolea majibu hayo wako nje ya
nchi kikazi.
KWA MAGUFULI KIMYA
NIPASHE lilipomtafuta Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, simu yake haikupatikana.
Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo, alisema hafahamu
lolote juu ya maendeleo ya kuundwa kwa kamati hiyo kwa kuwa yuko Mkoani
Tabora katika ziara ya Waziri Magufuli.
Alisema anatarajia kurudi Dar es Salaam wiki ijayo, na kumtaka mwandishi asubiri hadi atakaporudi ndipo atapata majibu sahihi.
Msemaji wa Wizara ya Uchukuzi, William Budoya, alipotafutwa alisema muda
uliopangwa na Waziri Mkuu bado haujaisha na kumtaka mwandishi awe
mvumilivu hadi kipindi kilichowekwa kitakapomalizika.
“Be patient (kuwa mvumilivu) mwezi ukikamilika tutawaeleza, kwa sasa ni mapema sana,” alisema Budoya.
Oktoba 9, mwaka huu mabasi yaendayo mikoani yaligoma kwa muda wa saa
sita baada ya kugomea maamuzi yaliyofanywa na Waziri Magufuli ya kufuta
msamaha wa tozo ya asilimia tano kwa wasafirishaji wa malori na mabasi
kwa uzito unaozidi. Tangazo la Waziri Magufuli lilisababisha vilio
kutoka kwa wasafirishaji na kufuatiwa na mgomo huo.
Hali hiyo ilimlazimisha Waziri Mkuu kuingilia kati na kutengua maamuzi
ya Waziri Magufuli na kuagiza kuundwa kwa timu ya kumaliza mgogoro huo.
Mvutano kati ya Wizara ya Ujenzi na wadau wa usafirishaji
ulisababishwa na kanuni ya 7 (3) ya Sheria ya usafirishaji ya mwaka 1973
ambayo Waziri Magufuli aliitumia kufanya maamuzi hayo.
Pinda wakati akitangaza uamuzi wa kusitisha tangazo la Waziri Magufuli,
alisema sababu ya mgogoro huo ilikuwa ni barua ya aliyekuwa Waziri wa
Miundombinu, Basil Mramba, ambayo aliiandika mwaka 2006 ya kutoa msamaha
kwa tozo kwa uzito wa magari uliozidi ndani ya asilimia tano ya uzito
unaokubaliwa kisheria.
Hata hivyo, alisema Waziri Magufuli aliamua kutumia sheria kwa kuwa mwongozo wa Mramba haukuwa wa kisheria.
ATHARI ZA MGOMO
Mgomo wa wasafirishaji ulisababisha Bandari ya Dar es Salaam kuelemewa kutokana na kuzidiwa mizigo.
Takribani tani 23,165 za mbolea ambazo zilikuwa zimeshushwa bandari hapo zilikwama kutokana na kutokuwapo kwa malori.
Sambamba na hilo, takribani meli tisa za mizigo zilikwama kushusha na kupakia mizigo bandarini.
Kadhalika, uwezo wa kushusha makontena katika bandari hiyo ulishuka kutoka makontena 800 kwa siku hadi 300. CHANZO:
NIPASHE
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment