BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA RAIS KIKWETE AAGIZA ASKARI WA WANYAMAPORI KUWAUA MAJANGIRI ILI KUGOMESHA UJANGILI NCHINI NA DUNIANI..

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiD1q7SnsWjzr77Astl1t5ZWuYfv7dgoWsKg0lDst7iZ5q06aPdEMaw4SHuS6yp7o5W4e09Z0n4nvt5JX-Q5sFA1-9LuMXDeh5_lW9vF8p3gTWhOhqhht_o6izVbXS6MwgUPRtsxpf10qWB/s1600/1185966_521022644618093_1339419024_n.jpgWANYAMA WAKIWA MBUNGANI


Balozi Khamisi Kagasheki. 
 
Na Seif Mangwangi, Arusha
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki amewaagiza askari wa wanyamapori kuwaua majangili pindi watakapowakamata ili kukomesha tatizo la ujangili nchini na duniani.

Akizungumza kwenye kilele cha matembezi ya kupinga mauaji ya tembo duniani katika maadhimisho yaliyofanyika jijini Arusha kitaifa, Kagasheki alisema kwa kauli yake hiyo anatarajia kupingwa vikali na watetezi wa haki za binadamu lakini hiyo ndiyo hali halisi.

“Ukiniuliza mimi nini cha kuwafanya majangili wanaoteketeza wanyamapori wetu nitakujibu kuwa wanatakiwa kuuawa huko huko wanapokamatwa na hii itasaidia kutokomeza kabisa jambo hili ambalo linamaliza wanyamapori wetu nchini na duniani,” alisema Balozi Kagasheki.

Alisema jangili yoyote akikutana na askari atakachofanya ili kujinasua ni kumuua askari hivyo ni wazi kutangulia kuwaua wao itakuwa ndiyo suluhu ya kupunguza mauaji ya wanyamapori nchini.  

Kagasheki aliwageukia wanasiasa na kusema wamekuwa sehemu ya kukwamisha jitihada za Serikali katika kupambana na ujangili kwa kuwatetea baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihusika kuteketeza wanyama hao.

Hata hivyo, alisema Serikali inalitambua hilo hivyo itapambana nao ili kuhakikisha suala la mapambano dhidi ya majangili linafanikiwa huku akiwasihi kufanya kazi ya siasa kama walivyoomba kwa wapiga kura wao.   

Kagasheki alisema ili kudhibiti ujangili nchini, Jeshi la Wanachi waTanzania (JWTZ) limejumuishwa kwenye mchakato wa mapambano dhidi ya majangili na kuwataka waliokuwepo kwenye matembezi hayo kujiandaa katika mapambano hayo na ambao hawajakuwepo wapelekewe salamu.

“Najua miongoni mwetu kuna majangili… napenda kuwaambia kuwa siku zenu sasa zimefika mwisho, na wale ambao hawapo wapelekeeni salamu, Serikali kupitia kwa Rais Kikwete imeamua kuliingiza jeshi kwenye mapambano ya kuokoa rasilimali wanyamapori na nina uhakika tutafanikiwa,” alisema.  

Akizungumzia sheria ambazo wamekuwa wakihukumiwa majangili, Waziri Kagasheki alisema wizara yake inatarajia kupeleka mabadiliko ya sheria hiyo bungeni ambayo itatoa adhabu kali kwa watakaokamatwa kwa ujangili.

“Adhabu wanayopewa mahakamani majangili ni sawa na utani kabisa,  ndiyo maana kila kukicha majangili wanaongezeka hivi sasa tumeamua kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria hii ili kutoa hukumu kali zaidi na kutokomeza tatizo la majangili nchini,” alisema Kagasheki.

Awali, akitoa salamu katika matembezi hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Utalii Tanzania (Tatoa), Willy Chambulo aliiomba Serikali kusitisha mchakato wa uwindaji wa wanyamapori kama tembo ili kukomesha tatizo hilo nchini.

Pia Chambulo aliiomba Serikali kuzungumza na nchi ambazo zimekuwa kinara wa ununuzi wa meno ya tembo ikiwemo China ili kushiriki kwenye mapambano dhidi ya mauaji ya mnyama huyo nchini na duniani. CHANZO http://jamboconcepts.com.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: