BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ZITTO KABWE KAMA KUTAJA MSHAHARA WA PINDA, WAZIRI NA MBUNGE NI KOSA BASI ACHUKULIWE HATUA KAMA YALIVYOFUNGIWA MAGAZETI !.


Naibu Katibu mkuu wa Chadema taifa, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mpanda katika viwanja vya maridadi hapo jana ambapo alikanusha uvumi ulionea kuwa amekuwa kimya na amepunguza makali yake bungeni kwa sababu amem

uoa mtoto wa Raisi kikwete alikana kumuoa mtoto wa kikwete.
 

AANZA NA KUKANUSHA UVUMI WA KUOA MTOTO WA JK.
Na Walter Mguluchuma.
Naibu katibu mkuu wa Taifa wa CHADEMA Zito Kabwe amekanusha uvumi ulioenea wa kuwa amemuowa mtoto wa Rais Kikwete na ndio maana amepunguza makali yake Bungeni ya kuuliza maswali na kuchangia hoja.

Zito alitowa kauli hiyo ya kukanusha uvumi wa kumwoa mtoto wa Rais Kikwete hapo juzi wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Maridadi mjini hapa

Alisema uko uvumi ambao umeenea hapa nchini kuwa makali yake yamekupungua bungeni kutokana na yeye kumuoa mtoto wa Rais Kikwete wakati sio kweli yeye hajamuowa mtoto wa Kikwete.

Alifafanua kuwa yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya kupigana ngumi bali yeye siku zote toka amekuwa mbunge amekuwa akipigania kutoa hoja zenye nguvu ndani ya Bunge kama hana hoja za msingi huwa hakulupuki ovyoovyo.

Alieleza ndio maana katika kikao kijacho cha Bunge ameisha wasilisha maombi ya mswada binafsi wa kupendekeza kufutwa kwa sheria ya mwaka 1976 sheria namba 3 ambayo amedai inavinyima haki na uhuru vyombo vya habari

Wako viongozi wamekuwa wakiitumia vibaya sheria hiyo na hasa pale wanapo kuwa wamekosolewa au kuandikwa vibaya na magazeti mbona mie Zito nilikuwa naandikwa vibaya na kusingiziwa kuwa nimejenga nyumba ya gorofa Dodoma wakati hata kiwanja sina Dodoma lakina hata siku moja sija vichukia vyombo vya habari alisema Zito

Alisema kitendo cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi ni ukiukwaji wa katiba kwani kila mwananchi ana haki ya kupata habari na kitendo hicho kinapunguza ajira kwa vijana

Alisema leo hii Serikali inapenda kufanya mambo yake kisiri na ndio maana hata mishahara yetu sisi wabunge ambao mmetuchagua nyinyi wananchi hamjuwi wakati ni haki yenu ngoja niwatajie mshara anao pata waziri na Wabunge.

Mshahara wa Mbunge kwa mwezi anapa kwa mwezi shilingi Tsh 11,200,000 wakati waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure kama ni kosa kutamka mshahara ni kosa basi namie nichukuliwe hatua kama magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge nitataja na Rais anapata mshahara kiasi gani kwa mwezi.

Kuhusu katiba aliomba marekebisho ya katiba yazingatie zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi kuliko viongozi kama ilivyo sasa na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri matokeo yake ni wananchi waliomchagua wanakosa uwakilishi bungeni

Alisema anao mfano hai kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi kuuliza swali hata moja bungeni kama kuna mtu anaushahidi wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi kuuliza yeye Zito yuko tayari kumpa shilingi laki mbili mwananchi huyo

Alifafanua kuwa Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza na aliteuliwa kuwa naibu wa Tamisemi hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda wote kuuliza maswali.

Mpanda Katavi yetu Blog
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: