
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar Es Salaam nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.
Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.
Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.
Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...? Credit: Tuangaze blog.

3 comments:
Inaonekana hujui ni vitu gani unaangalia pale unapochagua umpendaye tena wa kuishi nae pamoja. Mapenzi hayaangalii pesa, usharobaro wala ushamba kama unavyodai wewe. Kuwa serious na ujiulize unahitaji nini kwenye maisha yako ya mahusiano. Inawezekana huyo sharo unayemsema wewe anakuoenda kwasababu umeishatengenezwa na si kwamba ndio ana mapenzi ya kweli. Bt u know what?u will never know the value of what u have until you lose it. Be wise
We subiri risasi zako za kukutosha tu, mwehu mkubwa wewe!
wewe umejisahau tu, ukijikumbuka uatarudi kwake. Hata hivyo amshauri huyo kaka akuepuke kama ukoma, huna maana, akili na nidhamu.
Post a Comment