Polisi wakikagua gari walilokuwa wakisafiria watu wanne kabla ya
kushambuliwa kwa risasi na mtu alitajwa kuwa jina la Gabriel Munisi
aliyedaiwa kuua watu wawili na yeye kujiua baada ya kujeruhi wengine
jana asubuhi jirani na Club ya Wazee, Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha
ndogo polisi wakikagua silaha iliyotumika.Picha na Silvan Kiwale
DAR ES SALAAM.
MFANYABIASHARA wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
DAR ES SALAAM.
MFANYABIASHARA wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.
Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga
risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa
Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na
kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia
risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).
Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa
kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen
Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi
alisema Munisi alikutwa na bastola moja, magazini mbili na yalikutwa
maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili ambazo zilikuwa
hazijatumika.
Tukio hili limetokea mwezi mmoja baada ya
mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi na mzazi
mwenzake, Anthery Mushi.
Katika tukio hilo, Mushi alijiua baada ya kumuua
mama mzazi wa Ufoo na inaaminika pia tukio hilo lilisababishwa na
masuala ya mapenzi.
Lilivyotokea
Mashuhuda waliokuwapo katika tukio hilo walisema
mauaji hayo yalitokea saa 1.15 asubuhi baada ya Munisi kufika Ilala
Bungoni na kwenda katika Klabu ya Wazee iliyo jirani na eneo yalipotokea
mauaji na kunywa supu kabla ya kusogea karibu na lango la nyumba
anakoishi mchumba wake.
Mmoja wa majirani, Noel Gerald alisema alimuona Munisi akiwa amesimama karibu na lango la nyumbani kwa kina Christina.
Alisema baadaye waliona gari aina ya Toyota Hilux,
Surf, likitoka katika lango la nyumba hiyo na mara walimuona Munisi
akimwamuru dereva ashushe kioo lakini alikataa na kudai kwamba ndipo
alipoamua kuwapiga risasi waliokuwamo kwenye gari hilo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment