TORONTO, CanadaMEYA wa Jiji la Toronto nchini Canada, Rob Ford (pichani) ameomba msamaha kwa wananchi wake baada ya kukiri kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine.
Ford alisema kukiri kwa kile alichokitaja kuwa ni kosa lake ni jambo lililo gumu na lenye aibu ambalo amewahi kufanya huku akisisitiza kuwa hatajiuzulu.

Alisema kuwa pamoja na kutotaka kuomba msamaha pia ataendelea kufanya kampeni za kugombea nafasi hiyo mwaka ujao.
Kanda ya video inayomuonesha akitumia iliibuka Mei mwaka huu lakini awali Meya Ford alikana tuhuma hizo.
Wiki iliyopita, mkuu wa polisi mjini Toronto alisema aliipata nakala ya kanda hiyo ya video.
Hata hivyo, aliomba radhi na kusema anaipenda kazi yake na jiji hilo kubwa nchini humo huku akisema lilikuwa baya na kuwa wananchi hawana budi kurejesha imani yao kwake.
Alisema kuwa aliificha tabia yake kutoka kwa familia na wafanyakazi wenzake na kuwa yeye ndiyo wa kulaumiwa kwa hayo yote aliyofanya. JAMBOLEO

0 comments:
Post a Comment