Wanawake wa kabila la waturkana huko nchini Kenya.
SERIKALI ya Kenya imeripotiwa kutuma maafisa wa
polisi kuongeza ulinzi katika kijiji cha Lorokon kaskaskani mwa count ya
Turkana mahali ambapo watu wenye silaha walikuwa wamezingira vituo
vitatu vya polisi ambao pia inasemekana wamewateka wanavijiji.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema ugomvi wa mpaka baina ya jamii mbili za makabila ya waturkana na wapotok ndio chanzo cha tukio hilo.
Awali iliripotiwa kuwa watu wenye silaha kutoka jamii ya kabila la wapotok wamezingira kijiji cha Lorogon kwa siku nne.
Televisheni ya Kenya iliripoti mazungumzo ya kutatua mgogoro huo kati ya makabila hayo yanayogombana yalitarajiwa kufanyika siku ya jumapili.BBC
0 comments:
Post a Comment