MWENYEKITI wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania jana usiku
akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba
kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.
Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa
kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio
atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa
na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata
ndio kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club
ya Simba’.
‘Nimefurahi kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama
kwangu mimi, mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho
mchana makao makuu ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki
yangu mpenzi Zitto kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi
sijafurahia kwa hiyo siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage.
Alipoulizwa kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho
atakifanyiaje Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage
kasema swala la kocha atalizungumza leo ila hilo la kufanyia mkutano
na Waandishi wa habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na
wasiwasi kwani yeye ndio Mwenyekiti.
Kuhusu
kikao kilichofanyika na kumuondoa kwenye nafasi ya Uwenyekiti, Ismail
Aden Rage amesema kikao kilichofanyika sio halali manake ukisoma katiba
ya Simba, FIFA na CUF katika aya zote hakuna aya inayosema kamati ya
utendaji ina mamlaka ya kumsimamisha Rais au Mwenyekiti.
Baadhi ya Wanachama wa Simba wakicheza wakati wa mapokezi.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / KAMATI UTENDAJI YA KLABU YA SIMBA HAINA UBAVU KUMSIMAMISHA MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA ISMAIL ADEN RAGE, KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KUSIMAMISHWA KWAKE LEO SAA 7 MCHANA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment