
Kashfa za wabunge hao wa CCM zinatokana na hatua yao ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa nguvu na vijana wadogo.
Rosesweeter ambaye ana umri wa miaka 60, yuko katika kashfa ya kufunga ndoa na kinda wa miaka 26, Michael Christian, wakati Profesa Kapuya anahaha kujinasua na kashfa inayomzingira ya kumbaka binti wa miaka 16, ambaye sasa anatishia kumuua baada ya kumwaga mtama hadharani.
Ukija kwenye kashfa ya Rosesweeter kufunga ndoa na kijana wa miaka 26 sio kosa kisheria, lakini wadadisi wa mambo wanasema kimaadili ndoa hiyo haikupaswa kufungwa kutokana na umri wa bibi harusi kuwa mkubwa kiasi kwamba hana uwezo tena wa kuzaa wakati bwana harusi ndiyo kwanza kijana wa miaka 26 tu.
Wakati Profesa Kapuya anadaiwa kumbaka msichana huyo mwaka 2011, Rosesweeter naye alifunga ndoa na kijana huyo mwaka huo huo, Septemba Mosi. TANZANIA DAIMA.
0 comments:
Post a Comment