BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADIWANI WAMWAGIZA MKURUGENZI NA MWENYEKITI KUMTIMUA KAZI AFISA ELIMU TAALUM MBINGA MKOANI RUVUMA.

Baadhi ya madiwani wa Mbinga wakiwa katika Moja ya vikao vyao.


MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, wamewaagiza Mkurugenzi na  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kumwondoa Afisa Elimu taaluma wa halmashauri hiyo kwa madai ya kurudisha nyuma kiwango cha elimu katika wilaya hiyo.


Wametaka arejeshwe kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutokana na afisa huyo, Rashid Pilly, kudaiwa kuwa kikwazo katika utendaji kazi wa idara hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, Winfrida Kapinga, alisema baraza limekasirishwa na tuhuma zilizotolewa dhidi ya Afisa taaluma za kupanga kuendelea kuwarudisha nyuma kielimu, kutokana na kuona wivu na mikakati waliyoweka ya  kuongeza ufaulu.

Wilaya hiyo imeshika mkia kwa miaka mitatu mfululizo, ambapo baada ya Afisa elimu msingi wilaya, David Mkali, kuhamia wilayani Mbinga amefanikiwa kupandisha ufaulu kutoka asilimia 40 hadi 53.6 na  kuifanya halmashauri hiyo kushika nafasi ya pili kimkoa.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani mjini hapa juzi, Kapinga alisema kutokana na hali hiyo wameamua kumkataa Afisa taaluma huyo na kumrejesha kwenye mamlaka yake ya uteuzi ili kupunguza vurugu na migogoro ya kurudisha nyuma maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.


Alisema, Mkali alikuta wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu mwaka 2011 wakiwa 1744.
Mwaka 2012 idadi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ilipungua na kufikia 640 na mwaka huu idadi imepungua na kufikia 162 kitendo ambacho kimemfanya Afisa elimu taaluma kumwonea wivu na kuanza kuandika tuhuma za uongo kwa lengo la kumchafua Afisa mwenzie. 



Alisema, tangu mwezi Machi 2013 hadi Oktoba, mwaka huu kutokana na barua mbali mbali za tuhuma kuandikwa kwa Waziri Mkuu.
Pilly alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alisema kuwa amezisikia mitaani hajapewa taarifa rasmi kwa maandishi na kwamba yeye bado ni mtumishi wa serikali mpaka hapo atakapopata taarifa rasmi.

Alisema tuhuma za madiwani kuwa anakwamisha maendeleo ya elimu Mbinga siyo za kweli na kwamba wanaopaswa kulaumiwa ni walimu wakuu ambao ndiyo walikuwa wakiandika barua za malalamiko dhidi ya Mkali.
 

CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: