Home / Uncategories / MAJIGAMBO YA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI KUFUATIA KUTEKELEZA ILANI YA CCM NDANI YA MIAKA MITATU NDIYO HII BAADA YA KUCHAGULIWA 2010.
MAJIGAMBO YA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI KUFUATIA KUTEKELEZA ILANI YA CCM NDANI YA MIAKA MITATU NDIYO HII BAADA YA KUCHAGULIWA 2010.
ABOOD: NIMETEKELEZA ILANI YA CHAMA CHANGU CHA CCM HATUA KWA HATUA KATIKA JIMBO LANGU KWA KUTATUA KERO MBALIMBALI IKIWEMO KUSIMAMIA KIKAMILIFU MIRADI YA BARABARA, AFYA, KUVIWEZESHA VIKUNDI VIDOGOVIDOGO VYA WAJASILIAMALI, WANAUME KWA WANAWAKE, KUPUNGUZA KERO YA MAJI KWA BAADHI YA MAENEO KWA KUCHIMBA VISIMA .
NITAENDELEA HIVYO HIVYO KUWATUMIKIA WANANCHI WA JIMBO LANGU NA WATANZANIA KWA UJUMLA NIKISHIRIKIANA HALMASHAURI YANGU ILI WANANCHI WAFAIDIKE NA MATUNDA YA UONGOZI WANGU.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akieleza jambo wakati wa mkutano wake wa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM tangu achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2010, Abood alieleza mambo mbalimbali ikiwemo na kupunguza kero zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Fire Manispaa ya Morogoro. PHOTO/MTANDA BLOG.
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro naye akiwa ameungana na wananchi mbalimbali kusikiliza jambo katika mkutano huo.PHOTO/MTANDA BLOG.
Huyu jamaa alionekana kama ameona ile kitu ambayo huwa inabadilisha akili, kulia ni mmoja wa viongozi wa chama cha mapinduzi akimuonya jambo ambapo baadaye alimtoa eneo hilo kabla ya Mbunge wa jimbo hilo kueleza mambo aliyoyafanya ndani ya miaka mitatu baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.PHOTO/MTANDA BLOG.
Wana habari wa televisheni kutoka kushoto ni Michael Msillo ITV na Salum Mohamed Abood Media
Kada wa CCM kutoka ofisi ya umoja wa vijana makuu idara ya uhamasishaji, Juliana Chonza, akimwaga sera za chama hicho katika mkutano huo. kulia ni Dotto Kiswili
Diwani wa kata ya Nunge Fidelix Tailo kulia naye akifuatilia jambo sanjari na mwandishi wa HabariLeo John Nditi kushoto.PHOTO/MTANDA BLOG.
Mtangazaaji na Mwandishi wa Planet FM Morogoro, Anthony Mhando a.k.a Washngton DC akiwa na Kada wa CCM Juliana Chonza mara baada ya kada huyo kueleza sera za chama hicho katika mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment