DAR ES SALAAM.
WAFANYAKAZI wa Kariakoo jijini Dar es Salaam jana walifunga maduka yao kupinga utaratibu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa kutoza kodi kwa kutumia mashine za elektroniki (EFD).
WAFANYAKAZI wa Kariakoo jijini Dar es Salaam jana walifunga maduka yao kupinga utaratibu mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa kutoza kodi kwa kutumia mashine za elektroniki (EFD).
Wafanyabiashara walifanya mgomo huo ili
kushinikiza kuonana na ama Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha,
Dk William Mgimwa au Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Wanadai kuwa mashine hizo za EFD zinauzwa bei
ghali ya kati ya Sh800,000 hadi Sh1.2 milioni, gharama ya kuzifanyia
matengenezo zinapopata hitilafu ni kubwa na pia wanadai kuwa kuna harufu
wa ufisadi kwenye suala hizo kwa kuwa ni kampuni chache zilizochaguliwa
kuuza mashine hizo.
Maduka karibu yote hayakufunguliwa tangu alfajiri
tofauti na ilivyozoeleka na hata wafanyabiashara wachache waliojaribu
kufanya hivyo walilazimika kuyafunga kwa hofu ya kufanyiwa vurugu na
wenzao.
Baadhi ya maduka ya vifaa vya umeme, magodoro na
friji yaliyopo Mtaa wa Uhuru yalikuwa wazi lakini baada ya muda mfupi
yalifungwa.
Hata hivyo, maduka yaliyoko kwenye Soko Kuu la Kariakoo yalikuwa wazi muda wote.
Mgomo huo ulianza baada ya wafanyabiashara hao
kupeana taarifa wakihamasishana kutokufungua maduka yao kushinikiza
kusikitishwa kwa matumizi ya mashine hizo za kukokotoa kodi.
Msimamo wa Serikali.
Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema mgomo
wa wafanyabiashara wa Kariakoo hauwezi kubadili msimamo wa Serikali wa
kukusanya kodi kwa kutumia mashine za EFD. Alisema suala la bei haliwezi
kuwa kigezo cha kugoma kwa kuwa baada ya kununua fedha zao zitarejeshwa
kidogokidogo kwenye marejesho ya kodi.
“Changamoto iliyopo ni kwamba wafanyabiashara
wengi hawajui kama fedha hizo wanazonunulia mashine watarejeshewa kwenye
makato ya kodi. Hatuwezi kuzibadilisha mashine hizo kwa kuwa siyo kama
simu za mkononi, zimetengenezwa kwa mfumo maalumu wa TRA,” alisema.
Aliitaka TRA kuwaelimisha wafanyabiashara kuhusu manufaa ya kutumia mashine hizo.
TRA yakaza uzi. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment