BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI ZITTO ZUBERI KABWE AFUNGUA KESI YA KUTISHIWA MAISHA.

ZITTO KABWE AFUNGUA KESI KWA KUTISHIWA MAISHA KUFUATIA HEKAYA INAYOITWA 'RIPOTI YA SIRI YA ZITTO KABWE'.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amefungua mashtaka kwa madai kwamba anatishiwa maisha kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya siri ya Zitto Kabwe". 

Mbunge huyo amepost picha yake akiwa makao makuu ya polisi Dar es Salaam na kuandika maelezo yafuatyo kupitia ukurasa wake wa facebook:


"Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe". Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM. 
Wahusika waendelee kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani. Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa tuhuma za uongo.

Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa."NA GESTINA GEORGE.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: