Christina Newa.
DAR ES SALAAM.
IMEBAINIKA kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.
DAR ES SALAAM.
IMEBAINIKA kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.
Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana,
mmoja wa majeruhi ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo,
Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake, Gabriel
Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi kwa risasi yeye na mama yake mzazi,
Ellen Eliezer na kumuua mdogo wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na
kusaliti uchumba wao.
Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo
ni Christine kumkataa Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya
mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila
ambaye pia alifariki katika tukio hilo... “Kwanza Shumila hakuwa mchumba
wangu kama ilivyoelezwa. Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu
Caroline Newa. Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.”
Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na
Munisi katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu kubwa ya
maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisi mara kadhaa.
Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu
Munisi alikuwa akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma na alikuwa na
wivu uliopindukia.
Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya
kwenda kusoma katika Visiwa vya Cyprus kimyakimya pasi na kumuaga, jambo
ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka kisasi.
“Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi
akayapata na tukawasiliana na siku niliporejea alikuja kunipokea uwanja
wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake
akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza eneo la Kitangiri,” alisema na
kuongeza:
“Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”
“Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”
Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari
yao. Anasimulia kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote
na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye
dirisha na kuomba msaada kwa majirani na kuwapa namba za simu za ndugu
zake ili wamsaidie kuwapa taarifa.
Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na
polisi hatua iliyofanikisha msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam...
“Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha
huko.”
Baada ya kurudi Dar es Salaam, anasema Munisi naye
aliamua kumfuata lakini safari hii alifikia katika Hoteli ya MM
iliyotenganishwa na ukuta wa nyumba yao na akawa anafuatilia nyendo za
familia hiyo.
“Alikuwa ananitumia meseji kwamba amemuona dada
Caro, mama na Alpha na wakati mwingine anasema ameniona mimi mpaka nguo
tulizovaa, tukaanza kupata na wasiwasi,” alisema.
Wasiwasi huo ulitokana na historia ya maisha yao
ya Mwanza na pia tishio ambalo anadai kwamba Munisi aliwahi kulitoa
kwamba atahakikisha anaiteketeza familia yote kuanzia Goba anakoishi
mama yake (Ellen), Zanzibar anakoishi mdogo wake (marehemu Alpha) na
hapo Ilala. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment