Mbunge wa Iramba Maghariobi akiwatuliza wananchi wasiendelee kushangilia mafanikio yake aliyokuwa akiwaeleza hususani utekekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu Nchemba ametolea ufafanuzi wa Ujenzi wa Kituo cha kisasa cha afya kata ya Shelui wakati huo huo Mbunge huyo ametoa Gari la AMBULANCE kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa kata ya Shelui.
Kabla
ya kutoa taarifa ya kuwapatia gari ya Ambulance kwaajili ya
wagonjwa,Mbunge huyo amechangia mifuko 30 kwaajili ya ujenzi wa kituo
cha afya na huku akitoa mabati zaidi ya miatano kwaajili ya ujenzi wa
nyumba za Ibada na Vituo vya afya wilaya ya Iramba.
Hii
ni sehemu ya Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa hadhara
wa Mh.Mwigulu Nchemba kata ya shelui ndani ya jimbo lake la Iramba
magharibi.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa Iramba Mh.Mwigulu Nchemba amekabidhi dawati 20
kwaajili ya shule ya msingi moja wapo hapa Shelui.Kwa dawati hizi 20
Mbunge huyo atakuwa amefikisha dawati 60 ambazo wananchi waliomba
kwaajili ya kutatua swala la watoto wao kukaa chini kwa kukosa
Madawati.Lakini pia Mbunge huyo amepeleka madawati zaidi ya 100 kwenye
shule mbalimbali ndani ya jimbo lake kulingana na mahitaji ya shule
husika.
Mtendaji
wa serikali ya Mtaa wa Shelui(kushoto) wakiwaonesha Wananchi moja ya
Dawati zuri na imara sana ambazo Mh.Mwigulu nchemba ametoa kwaajili ya
shule ya msingi hapa Shelui.
Kwenye
Mkutano huu wa hadhara.Mh.Mwigulu nchemba alitoa fursa kwa wananchi
wake kuuliza maswali mbalimbali yanayohusu mambo ya maendeeleo ndani ya
kata na jimbo lake la Iramba.Huyu ni mmoja wa vijana aliyejitokeza kutoa
shukrani zake kwa Mbunge wake kwanamna alivyomsaidia kutatua matatizo
yake na familia yake.Kijana huyu amewaomba wanashelui kutoa ushirikiano
wa kutosha kwa Mbunge wao kwasababu amekuwa bega kwa bega katika
kushughulikia matatizo yao.lakini pia kijana huyu alitumia muda wake
kuwaelimisha wananchi wa shelui kuwa na tabia ya kuhoji matumizi ya
fedha za Mfuko wa bunge na michango mbalimbali(mapato na matumizi).
Ilikuwa
ni furaha kwa Mwigulu nchemba kuzungumza na wananchi wake kuhusu
maendeleo anayowafanyia,Picha hii imepigwa wakati anacheza wimbo wa
kinyiramba kufurahia namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi
kumsikiliza kwenye mkutano wake,.
Huu ni upande mwingine wa wananchi waliofika kusikiliza mkutano wa Mbunge wao Mh.mwigulu nchemba.
Mh.Mwigulu
Nchemba amewasisitizia sana wananchi wa Shelui na Iramba kushiriki
kwenye kazi za maendeleo,Kuachana kabisa na kumtegemea Mbunge kufanya
kila kitu.Pia amewaomba kuhakikisha wanasimamia kidete miradi mbalimbali
inayoendelea kutekelezwa ndani ya wilaya yake.Pia amewaomba vijana
kujitokeza kwenye chaguzi mbalimbali mwaka ujao kwenye serikali za
mitaa,Ameyasema hayo kwa kuzingatia kuwa sehemu kubwa ya wananchi wa
sasa ni vijana,hivyoi vijana wana fursa ya kushiriki kwenye kazi za
maendeleo kwa wingi sana,na endapo watashiriki kwenye chaguzi watakuwa
wamejiwekea mazingira mazuri yakuja kuwa viongozi wakubwa baadae.
Mh.Mwigulu
Nchemba akiteta jambo na Mwananchi wake akieleka kwenye jukwaa kwaajili
ya kuzungmza na wananchi wake wa kata ya Shelui.
Na Mwandishi Wetu.
Naibu katibu CCM Tanzania Bara na Mbunge
wa Iramba Mgharibi Mh.Mwigulu Nchemba leo jumapili 3/11/2013 amefanya
mkutano mkubwa wa hadhara hapa Iramba kata ya Shelui akizungumza na
wananchi wake kuhusu shughuli mbalimbali za maendeleo na kukabidhi
madawati kwaajili ya shule pamoja na kutoa taarifa ya kununua Ambulance
kwaajili ya wanaShelui ya matumizi ya kubebea wagonjwa kituo cha afya
cha Shelui.
Mbunge huyo ambaye kwa muda mrefu sasa
ameteka media za nchi kutokana na umahili wake wa kisiasa,akiwa
amembatana na Mbunge wa Tabora Mjini amezungumza mambo mengi sana na
wanashelui ikiwa pamoja na kuwapa nafasi ya kuhoji na kuuliza maswali
mbalimbali ya mwendeo wa siasa na utekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwigulu
Nchemba amewapongeza sana wakazi na wananchi wa Shelui kwa namna
walivyoshiriki kwenye ujenzi wa kituo cha afya ambacho yeye(mwigulu)
amechangia mifuko ya cement na mabati.
Pia kwa sasa amewanunulia gari la
Ambulance kwaajilya wagonjwa,Gari lipo mbioni kuletwa Shelui mapema
ndani ya Mwaka huu.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo
amewaomba Wanashelui kupuuzia kelele zozote za wapinzai za kuhusu
yeye,amedai kuwa wapinzani(CHADEMA) wameelekeza nguvu zao kupambana na
yeye kwasababu ni tishio kwao na amekuwa mstari wa mbele kufichua maovu
wanayofanya na kupanga kuyafanya.
Hivyo yeye yupo imara sana na
anategemea wananchi wa Shelui hawatatoa nafasi kwa watu waaina hiyo ya
CHADEMA.Mwigulu amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwapa nafasi wapinzani
nikukaribisha vurugu,uvunjifu wa Amani katika kata yao,Wapinzani ndani
ya vyama vyao wanapigana ngumi mwenyekiti kwa mwneyekiti na mmeona namna
walivyosababisha kifo cha kijana pale Ndago,walivyomwagia tindikali
kijana(Musa Tesha)pale Igunga n.k.alisema Mwigulu.
Vijana endeleeni kujishughulisha na kazi
za maendeleo,endeleeni kujikusanya kwaajili ya kutoa misaada ya
bodaboda na mikopo kama nilivyofanya kwenye kata zingine,Naomba mshiriki
kwenye michezo hasa hii michuano yangu niliyoanzisha.Kukaa bila kazi ni
hatari sana kwa kijana ndio maana mnakuja kujiingiza kwenye vyama
visivyo na mwelekeo wowote hapa nchini"Mwigulu.
Jambo kubwa la kufurahisha katika
Mkutano huu Mh.Mwigulu Nchemba alitoa nafasi kwa wananchi kutoa dukuduku
zao,mawazo na maswali ya mambo mbalimbali yanayowakabili.Maswali yote
yalijibiwa na mengine kujibiwa na watendaji moja kwa moja,Hatua hii
imetoa fursa kwa wananchi kujua mambo mengi hasa matumizi ya mfuko wa
jimbo ambapo wengi wao walikuwa hawajui kuwa Mbunge hakutani na fedha ya
Mfuko wa jimbo zaidi ya Ofisi ya waziri mkuu na mkurugenzi wa wilaya na
kisha kwenda kwa mfumo wa cheki kwenye serikali za vijiji.
0 comments:
Post a Comment