BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WABUNGE KANDA YA ZIWA WASHTAKIWA KATIKA BARAZA LA MAADILI.

Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli.

DAR ES SALAAM.
WABUNGE watatu na madiwani wawili wa Kanda ya Ziwa, wameshtakiwa mbele ya Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma.


Viongozi hao pamoja na wanasheria watatu, akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Sengerema Liveti Msangi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha wanasomewa tuhuma zao hizo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Balozi, Jaji Mstaafu Hamis Msumi na wajumbe wawili wa baraza hilo, Hilda Gondwe na Celina Wambura.

Akizungumza na waandishi wa habari Nov 15 mwaka huu, Kaimu Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tixon Nzunda alisema baraza hilo linaendelea kusikiliza kesi hizo mkoani Tabora, ambapo wananchi wanaruhusiwa kusikiliza kesi hizo huku Sekretarieti hiyo ndiyo mlalamikaji. 


“Kama nilivyosema ni baraza la wazi, ni viongozi mbalimbali walioshtakiwa huko, lakini kwa kuwa mimi simo miongoni mwa wanaoendesha kesi hizo sipo tayari kuwatajia,” alisema Nzunda.

Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika vyanzo vyetu vya habari, wabunge hao wametajwa kuwa ni Lameck Airo (Rorya), Salvatory Machemli (Ukerewe) na Suleiman Suleiman (Kishapu).

Madiwani wanaoshtakiwa kwenye baraza hilo ni Mathias Bisoma (Kata ya Kanazi, Kagera), Meya wa Jiji la Mwanza Henry Matata ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitangiri.

Viogozi wengine walioshtakiwa na Sekretarieti ya Maadili katika Baraza hilo ni Mwandishi Mkuu wa Sheria, Casmir Sumba Kyuki na Mkurugenzi Msaidizi Uandishi wa Sheria, Sarah Kinyamfura Barahomoka.

Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili viongozi hao ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, huku wengine wakidaiwa kushindwa kuwasilisha matamko ya rasilimali zao.

Awali, Nzunda alifafanua kuwa kesi hizo zitasikilizwa kwa wiki mbili, ambapo mashahidi ni wananchi. Baraza hilo ni taasisi huru inafanya kazi zake kwa mara ya kwanza baada ya kuchanguliwa na kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Julai mwaka huu. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: