Mwenyekiti wa Klabu ya Obama Group Dkt. Mwena Issa Omar aliyevaa miwani na Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (NCD) Omar Mwalim Omar wakiongoza mandamano katika madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani,yaliofanyika viwanja cha Maisara Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa mazoezi kutoka Klabu ya Obama Group Fatawi Haji Mussa akiongoza mazoezi kutoka Vilabu mbalimbali vya Mjini Zanzibar katika madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani,yaliofanyika viwanja cha Maisara Mjini Zanzibar.
Wasani wa Kikundi cha Black Roots wakiongozwa na Makombora wakionyesha igizo lenye ujumbe wa athari za ulaji wa halua na uvutaji sigara kwa wagonjwa wa Kisukari katika madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani ambapo kwa Zanzibar yalifanyika Maisara Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Juma Duni Haji akiwahutubia wananchi katika madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani iliofanyika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

0 comments:
Post a Comment