BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BARAZA LA MADIWANI JIJI LA MBEYA KUWABURUZA MADIWANI WA CHADEMA MAHAKAMANI.

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2010/07/Chadema2.jpg 
BARAZA la Madiwani jijini Mbeya, juzi lilipitisha maamuzi ya kuwaburuza mahakamani madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). 




Madiwani hao ni wale ambao watabainika kughushi sahihi za wenzao ikiwemo ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi ili kuitisha kikao cha kujadili bajeti na wale watakaobainika kuwashambulia madiwani wa CCM. 



Mwishoni mwa wiki, kilifanyika kikao cha kawaida cha baraza hilo ambapo baadhi ya madiwani wa CHADEMA walihoji majibu ya barua waliyoandika na kuweka sahihi zao wakitaka kikao cha kujadili bajeti iliyotumika kuwapeleka wajumbe wa jiji hilo na Mstahiki Meya kwenda nchini China bila ridhaa yao. 



Kutokana na swali hilo, waandishi wa habari walitolewa nje wakati Mstahiki Meya Athanas Kapunga, akijibu swali hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya kikao kutokana na mashaka yaliyopo kwenye sahihi za wajumbe. 



Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao hicho, Mstahiki Kapunga alisema uchunguzi wa awali umebaini baadhi ya sahihi ni za kughushi ikiwemo ya Bw. Mbilinyi hivyo barua hiyo kukosa sifa ya kushughulikiwa.



Alitolea mfano wa madiwani ambao saini zao zinadaiwa kughushiwa kuwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Forest, Bw. Boyd Mwabulanga ambaye yuko jijini Dar es Salaam kwa matibabu baada ya kuvunjika mguu kwenye ajali na Bw. Mbilinyi ambaye wakati huo alikuwa na udhuru nje ya nchi kwa shughuli za kibunge.



Alisema pamoja na kutoa majibu hayo, baadhi ya madiwani wa CHADEMA waliamua kuanzisha vurugu za wazi kwa kuwashambulia wenzao wa CCM kwa matusi na kutoka nje ya ukumbi na wenzao kuwafuata ili kujibu mapigo lakini polisi waliingilia kati. 




Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo baraza limemwagiza Mwanasheria wa Jiji kukamilisha uchunguzi wa jambo hilo na kutengeneza mashtaka dhidi ya madiwani ili waweze kufikishwa katika Kamati ya Maadili na wale ambao watabainika kughushiwa sahihi watakabiliwa na kesi ya jinai. 



“Mimi kama kiongozi mzoefu, siwezi kuona baraza langu linakosa maadili, nitahakikisha madiwani hao wanachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kudhalilisha wenzao kwenye vikao,” alisema.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: