DK SLAA ATUMIA BUSARA KWA KUWAZUIA POLISI KUTOCHANA MABANGO YENYE UJUMBE KATIKA MKUTANO WAKE WA CHADEMA KASURU MKOANI KIGOMA.
“Polisi wangu nawaomba sana msiendelee kuchana mabango ya hao vijana wala msihangaike nao kuwazuia wasije hapa, tena ningependa kuwaona, waacheni wasogee hapa mbele ya watu wote.
“Vijana wangu hebu sogeeni hapa mbele kabisa ya jukwaa mkae hapa, kaeni hapa niwaone na nisome mlichoandika maana huko sioni mabango yenu yameandikwa nini,” alisema Dk. Slaa huku vijana hao wakitii amri hiyo.
“Najua watu wengi mlishangaa nilipowazuia wale polisi wangu wasiendelee kuwazuia hawa wasije hapa mkutanoni na wasichane mabango yao.
“Haya mambo tulijua kuwa yangelikuwepo. Hayatusumbui kabisa. Naomba wananchi wangu kama mlivyoshangilia muwasikitikie tu hawa vijana maana hawajui wanachokifanya. Hebu ngoja niwaulize vijana wangu.”
“Chama hiki ni cha kidemokrasia, wala wasiwapatie taabu. Tunajua kuwa hayo yapo,” alisema Dk. Slaa.
huyu ndo rais mtarajiwaamejaa busara sana.
0 comments:
Post a Comment