Maelezo ya awali kutoka Bangui yanaeleza watu kadhaa waliuwawa Alhamisi katika mapigano katika sehemu tatu za mji ikiwa ni pamoja na mtaa wa Boy Rabe.
Msemaji wa rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia amewashutumu waunga mkono wa rais wa zamani Francois Bozize.
Mmoja wa wanafunzi mjini hapo, Wilfreed Koyamba amesema watu wana wasi wasi kwa usalama wao na kujiuliza ni lini msaada utafika.
Anasema jeshi la Ufaransa liliwambia siku tatu au nne zilizopita kwamba wako mpakani na wanasubiri kupata idhini ya kuingia, lakini hadi hivi sasa hawajaonekana.
Baraza la Usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kupiga kura Alhamisi juu ya azimio litakalo ruhusu mataifa ya Kiafrika na Ufaransa kupeleka wanajeshi zaidi huko CAR.http://www.voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment