BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAYA NDIYO MAMBO YASABABISHAYO WATOTO KUZALIWA NA MTINDIO WA UBONGO.


NI ajabu kuona wanadamu wanakuwa wabaguzi kwa kiasi hiki kwa sababu ya maumbile. Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la mtindio wa ubongo, hali ambayo imekuwa ikisababisha jamii mbalimbali kuwanyapaa na hata kuwabagua watoto wenye tatizo hilo.



Kitaalamu, mtindio wa ubongo unaelezwa kuwa ni hali inayompata mwanadamu kwa ubongo wake kushindwa kufanya kazi katika utaratibu wa kawaida. Kimsingi, ni uwezo wa ubongo kutokukua vizuri na kushindwa kufanya kazi yake katika mazingira yake ya kawaida.


Wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania wanabainisha kuwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, si kwamba ana matatizo ya akili ama mtindio wa ubongo.


Mtindio wa ubongo unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwamo ubongo kuathirika wakati wa kuzaliwa, na hata maisha ya utoto.


Kumbe, yapo mambo matatu yanayosababisha matatizo kwenye ubongo wa mtoto ambaye hajazaliwa mfano ugonjwa wa down syndrome hujitokeza baada ya matatizo katika vinasaba kutokea ambayo baadhi ya matumizi ya dawa husababisha mabadiliko katika vinasaba kama vile dawa za kunywa, ulevi kupindukia (fetal alcohol syndrome) na kuwa na mwili wenye afya dhaifu (fragile X).


Viasili, wakati mwingine huwa ni matokeo ya mtindio wa ubongo. Hiyo hutokana na asili ya kifamilia kuwa inapotokea mmoja wa wanafamilia wana asili na hali hiyo, basi wengine miongoni mwao watapata.


Mbali na hayo, pia matumizi ya dawa kali anazotumia mama wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa za kulevya, pombe, hali ya hewa, au hata ajali husababisha kufikwa na hali hiyo.


Utafiti uliowahi kufanywa katika sehemu mbalimbali, unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayopata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS).


Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida (facial deformities). Kwa mfano, watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.


Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne.

Hata hivyo, dalili zifuatazo zinaashiria kuwa mtoto ana tatizo hili.
Kwanza, haonyeshi dalili yoyote ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka, kwa maana kwamba hata kama kuna vitu vya kuchezea hawezi kujishughulisha navyo.


Pia, ni vigumu sana kufundishika na hata kujifunza kusoma huwa ni kazi ngumu ukilinganisha na watoto wa rika lake, hawezi kula mwenyewe, kuvaa mwenyewe au kujifunza kutumia choo.


Zipo dalili nyingi zinazoweza kujitokeza na mara nyingi zinatambuliwa na madaktari maalum wa watoto.


Mtindio wa ubongo na ulemavu wa akili
Mtaalam wa masuala ya mtindio na ulemavu wa akili,
anasema katika mahojiano maalumu kuwa watoto wenye matatizo hayo wako wa aina mbili. Watoto wenye mtindio na ulemavu wa akili. 



Anasema kuwa tatizo hilo linazidiana kwa kuwa, wapo watoto wenye ulemavu wa akili na wenye mtindio wa ubongo kwa wakati mmoja na wapo wenye matatizo ya mtindio na wenye ulemavu.
Aina hizo tatu zinatofautiana; mtoto aliyeharibika mota ya ubongo kwa kiasi kikubwa hupatwa na mtindio wa ubongo. 



Kama mtoto atakuwa ametindia upande wa kushoto, madhara yataonekana upande wa kulia kwa mtoto kuburuza mguu na mkono kutofanya kazi na hivyo hivyo endapo itatokea kwa upande mwingine, Wakati mwingine husababisha ugonjwa wa kifafa kwa mtoto.


Tatizo lingine linakuja, ikiwa mota ya fahamu haikuharibika, basi mtoto atapatwa na ulemavu wa viungo.
Mbali na dalili za awali, mtoto anakuwa na dalili za hali hiyo na wakati mwingine chanzo chake ni uvutaji sigara kwa mama mjamzito.


Hii pia husababisha mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuwa na kichwa kidogo, na kutounga uti wa mgongo. Pia aina ya vyakula anavyokula mama. 



Kisababishi kingine cha mtindio wa ubongo, ni pale mama anapochelewa kupata huduma ya uzazi anapofikia hatua ya kujifungua ama wauguzi kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya kubaini njia ya uzazi kushindwa kufunguka na uzazi zaidi ya miaka 35.


Hata hivyo, utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Emory cha Atlanta, Marekani katika Kitivo cha Dawa, unabainisha kuwa baadhi ya watoto wenye mtindio wa ubongo wanafundishika.
Inaelezwa pia kwamba, watoto hawa wanaweza kubadilika, iwapo tu watafundishwa kwa makini, utulivu na uvumilivu mkubwa.
Mtu anayemfundisha mtoto wa aina hii hatakiwi kamwe kuwa na hasira, na pia inashauriwa sana kuwapongeza wanapofanya vizuri japo kidogo.


Mwalimu anatakiwa awe mpole na ufundishaji wake usiwe wa haraka haraka, aonyeshe mapenzi kwa mtoto, hapaswi kumkemea hata kama anakosea. “Utakuta mwingine hacheki, au anatoka udenda lakini kama akicheza akili inajitengeneza na inaweza kufikia mate yanakatika na hata kucheka na wakati mwingine hurudi katika hali ya kawaida,” anasema.


Watoto wa aina hii inashauriwa wapewe nafasi ya kujenga urafiki na watoto wenzao wa rika lao.


Awali, watoto wenye matatizo ya akili walikuwa wanatengwa na watoto wenzao katika madarasa, kwa kuwekwa kwenye madarasa maalum.


Siku hizi inashauriwa kuwa watoto hao wachanganywe na wanafunzi wenzao wasio na matatizo ya akili, japo hata kwa nusu siku. Utaratibu huu hujulikana kitaalamu, mainstreaming.


Mbali na hayo, inaelezwa pia kuwa wakati mwingine watoto kabla ya kufikwa na hali hiyo ya ulemavu wa akili, wakati mwingine huzaliwa njiti (premature) ambayo mara nyingi mtoto huwa na udhaifu wa viungo.


Matatizo ya uzazi, na uzazi usio salama hufanya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na hiyo husababisha ulemavu wa akili kwani wakati mwingine ukuaji wa ubongo hauwi katika mazingira ya kawaida.


Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Children, Steve Thorn anasema watoto 210,000 huzaliwa kila mwaka na watoto wa kiume ama hufa au kupata ulemavu kwa kuzaliwa kabla ya wakati.


Anasema kwa mwaka jana pekee, watoto wa kiume njiti 114,000 walizaliwa ikilinganisha watoto wa kike 97,000 na kuongeza idadi ya vifo ama wakati mwingine kupatwa na matatizo ya upofu, uziwi na mtindio wa ubongo.


Dk Daphne Austin wa Mtandao wa Kamisheni ya Afya ya Jamii Uingereza anasema hana shaka kuwa watoto njiti hukua vizuri hadi kufikia wiki 23, 24 na 25 lakini wengi wao hupatwa na ulemavu wa viungo na ubongo. http://manyandahealthy.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: