BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DEREVA WA BASI LA SIMIYU EXPRESS AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO KUPATA AJALI IHUMWA MKOANI DODOMA.


Hii kati ya ajali ambazo zimekuwa zikitokea kila mara Tanzania.


WATU wawili wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi waliolokuwa wakisafiria la Simiyu Express kupinduka katika eneo la Ihumwa nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.



Basi hilo lenye namba za usajili T 717 ANL aina ya scania basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Mramba Issa (31).


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Susan Kaganda, alisema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Bariadi kwenda Dar es salaam likiwa na abiria 60 liliacha njia na kupinduka kutokana na mwendo kasi . 


Kamanda alisema kwamba ajali hiyo ilitokea leo alfajiri majira ya saa tisa usiku katika barabara ya Dodoma-Dar es salaam eneo la Elshadai . 


Kamanda Kaganda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva wa basi hilo Mramba Issa mkazi wa Magomeni Dar es salaam na Frola Erenest(21) Mwalimu wa shule ya msingi Mwamoto kolokolo, Bariadi. Aidha kamanda akizungumzia zaidi ajali hiyo alisema kwamba basi hilo lilikuwa likiwakwepa askari wa barabarani kwa kupita njia za panya. 


Alifafanua kuwa kwa basi hilo kusafiri usiku huo ni kukwepa askari . Aliwataka pia wamiliki wa magari kuweka madereva wawili kwa magari ya masafa marefu na pia wazingatie sheria za barabarani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: