HAYA NDIYO MAWAZO YA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI ZITTO KABWE JUU YA UHURU WA TANZANIA BAADA YA KUTIMIZA MIAKA 52, TUMEKOSEA HAPA.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Dar es Salaam,Tanzania
Matumaini yalikuwa makubwa sana mwaka 1961 Taifa letu lilipojikomboa kutoka makucha ya ukoloni. Vita 3 - Umasikini, Ujinga na Maradhi zilitangazwa. Azimio la Arusha likawa tumaini kubwa la kutokomeza umasikini, hasa wa vijijini.
Ni kweli tumepiga hatua kwenye Nyanja kadhaa. Ni dhahiri kuwa kwenye maeneo mengi tumerudi nyuma sana. Uwezo wetu wa kuzalisha Mali na kuondoa umasikini umepungua ambapo sasa uchumi unakua kwa wastani wa asilimia 7 lakini umasikini haupungui kwa sababu sekta ya wanyonge-kilimo, imedumaa.
Takribani mazao yetu yote ya kilimo tunauza nje kama ghafi tofauti na miaka ya 1970 ambapo tulianza kuongeza thamani kama Korosho, Kahawa, Pamba na Katani. Tumerudishwa nyuma na ubinafsishaji na menejimenti za hovyo hovyo.
Elimu sasa ni bora elimu na sio elimu bora maana watoto hawajifunzi mashuleni na hata wahitimu wa vyuo vikuu uwezo wao kukabili changamoto za nchi makazini ni mdogo sana.
Afya ya wananchi bado mbaya kutokana na wananchi wengi kufariki kwa magonjwa yanayotibika. Miaka 52 baada ya Uhuru ni asilimia 6 ya Watanzania wana hifadhi ya jamii.
Wakulima wetu bado hawana bima ya mazao yao wala pensheni. Changamoto ya kizazi cha sasa cha viongozi ni ku transform nchi ili kuongeza uwezo wa uzalishaji, kuongeza ajira, kupunguza inequality na kujenga Taifa imara mbele ya mataifa.
http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment