DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara ameitaka Serikali iwaruhusu kufanya mikutano ya hadhara vinginevyo watafanya maandamano makubwa Desemba 22 mwaka huu.
Akizungumzia na mwandishi wa habari hizi, Bungara
alisema ni jambo la kushangaza kuendea kuzuiwa kuwasiliana na wananchi
wao bila sababu yoyote ya msingi.
Aliongeza kuwa tangu wafungiwe kutokana na vurugu
zilizotokana na uvumbuzi wa gesi asilia Mtwara hadi leo, hawaruhusiwi
kufanya mikutano hiyo.
Alisema tayari wameshaandika barua tatu kwa Jeshi la Polisi kuomba mikutano hiyo iendelee, lakini haijazaa matunda.
Alisema barua hizo ni zenye kumbukumbu namba
CUF/KL/K/M/3/51/ kuomba tarehe ya kufanya mikutano ya hadhara lakini
hawakuruhusiwa.
Alisema walijibiwa na jeshi hilo kupitia barua
kumbukumbu namba vol.11/149 inayosema Marufuku kwa Vyama na Dini zote
kufanya mikesha, maandamano na mikutano ya hadhara isipokuwa mikutano ya
ndani tu kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kutokana na hali hiyo, walilalamikia hatua ya
kutozungumza na wananchi wao na kuwaleza utekelezaji wa ilani ya chama
pamoja na maendeleo. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment