DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati
ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu
wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana
wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti
hili kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea
tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri
akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani
ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu
mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana
naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.
“Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, …. nadhani
hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi,
pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje
wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto… wanajua siwezi kusemea nje
maana sina kinga…, hivyo wanataka kuniondoa bungeni…” alisema.
Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni
kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika
kipindi chake chote cha kisiasa.
Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima
wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya
mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na
mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.
“Je, mbunge anayetumika na Chama Cha Mapinduzi
anaweza kupeleka hoja ya kumng’oa Waziri Mkuu na kumshinikiza Rais mpaka
akasimamisha kazi mawaziri wanane? Je, mbunge anayetumika anaweza
kushikia bango watu wanaotorosha fedha nje ya nchi?” alihoji Zitto.
Tuhuma za usaliti
“Sizijui hizo tuhuma 11 kwa sababu nilichoelezwa
kwenye kikao cha Kamati Kuu sicho kilichoelezwa na chama kwenye mkutano
wake na waandishi wa habari… hivyo sijui kabisa hizo tuhuma zangu ni
zipi mpaka sasa,” alisema.
Alisema kuwa kwenye Kamati Kuu alilaumiwa kwa
masuala matatu. Akizitaja: “Nililaumiwa kuwa sifanyi kazi za chama, la
pili kuwa nimemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akague vyama
kutokana na kuwa na nia mbaya na chama hicho.
Tuhuma ya tatu ni ile ya kukataa kupokea posho bungeni ambapo nadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzangu.” MWANANCHI.
Tuhuma ya tatu ni ile ya kukataa kupokea posho bungeni ambapo nadaiwa kulenga kuwadhalilisha wabunge wenzangu.” MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment