Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu. Picha na Maktaba.
KAMBI ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
KAMBI ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa
nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia
mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema
Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa
maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe
iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu,
Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.
Kwa mujibu wa habari hizo, katika Mkutano wa 14 wa
Bunge unaoanza leo, kambi rasmi ya upinzani imepanga kumvua rasmi Zitto
nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha.
Jana, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu alithibitisha kuwapo kwa mpango wa mabadiliko hayo na kwamba
yanatarajiwa kufanyika kati ya mwishoni mwa wiki hii na mwanzoni mwa
wiki ijayo.
“Tutakaa mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa
wiki ijayo kwa sababu Kiongozi wa Kambi (Freeman Mbowe), atafika bungeni
Desemba 6, mwaka huu na ndiye Mwenyekiti wa Baraza Kivuli,” alisema
Lissu na kuongeza:
“Mbali ya Zitto kuna Said Arfi (Mbunge wa Mpanda
Mjini) ambaye amejiuzulu nafasi zake zote ikiwa ni pamoja na Waziri
Kivuli wa Uchukuzi na tutaangalia ufanisi wa mawaziri wengine kivuli”.
Baraza kivuli linaundwa na mawaziri 18 wakiongozwa na Mbowe na Zitto aliyekuwa Naibu wake na Manaibu saba.
Kujitoa kwa wanachama
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki,
alisema angeogopa kama kungekuwa na wimbi la wanachama zaidi ya 1,000
kuondoka katika chama kupinga misingi ya chama.
“Lakini kama walimfuata Zitto ndani ya chama ni
ruksa sisi hatuna shida lakini kama ni chama hapo kuna la kuangalia…
Sisi tunaamini wanachama wetu hawafuati mtu, bali misingi,” alisema. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment