BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

OFISI YA WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANDA PETER PINDA YAINGIA KATIKA KASHFA YA UFISADI WA Sh2.3 BILIONI,CCM IKIFICHUA UOZO HUO.

 
RUJEWA. 
OFISI ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye kashfa ya ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya viongozi wa CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa hiyo ilitokea mwaka 2011/12.



Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.


Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.


Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo.


Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: