BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROFESA WA RAIS JAKAYA KIKWETE AKATAA KABISA KUITWA MZIGO.

 
WAZIRI wa Maji, Profesa Maghembe, amesema siyo mzigo kwa serikali kwa kuwa amekuwa anatimiza wajibu wake sawasawa.


Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kufutia habari iliyoongoza ukurasa wa kwanza katika gazeti  hili Jumatatu wiki hii ikisema: “ Ni wiki ya majanga kwa Maghembe, Chiza, Malima” ikielezea kuwa malalamiko yaliyoelezwa dhidi yao kuhusu udhadifu wa utendaji wao yataibuliwa bungeni wiki hii, Profesa Maghembe alisema kuwa suala linalozungumziwa halimuhusu kwani chimbuko la malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Ruvuma ni zao la korosho ambalo haliko wizarani kwake.

Profesa Maghembe alisema kuwa amezungumza na Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye alimuhakikishia kuwa katika mawaziri aliotaja kuwa wanakwaza CCM na kutaka waitwe mbele ya Kamati Kuu kuhojiwa kwa kuwa hawatekelezi ilani ya chama hicho, jina lake halikuwako.

Hata hivyo, Maghembe alipoelezwa kuwa Nape kwenye mkutano wa viongozi wa sektretariati ya CCM walioko ziarani mikoa ya nyanda za juu kusini wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alisema alimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kama amemewahi kuwaona Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza au Naibu wake, Adam Malima, mkoani humo kutatua kero za wakulima wa korosho, alisema hajawahi kuwaona na hata mtangulizi wao, kwa  maana ya Profesa Maghembe naye hakuwahi kifika Ruvuma, alisisitiza kuwa hakuna waziri mwenye uwezo wa kufika kila wilaya ya Tanzania katika kupindi cha miaka mitano.

“Haya madai ni ya ajabu sana. Mimi nimekaa pale Kilimo kwa miezi 13 tu, sasa huyu anayesema kuwa waziri ni lazima afike kwenye kila wilaya ya Tanzania sijui anazungumzia nini.

Kwanza ni lazima watu wajue hata korosho zinazozungumziwa hazilimwi mkoa mmoja tu, kuna mikoa mitano inalima korosho, kwa hiyo kutokufika Ruvuma tu haikiwezi kuwa ndiyo kigezo pekee cha kupima utenedaji wa mtu.” alisema.

Habari iliyoandikwa Jumatatu wiki hii na NIPASHE ilikuwa inaelezea kusudio la wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) la kuwataka wabunge wenzao wa CCM wawaunge mkono kwenye mkutano wa  14 wa Bunge ulioanza jana ili kuwawajibisha mawaziri ambao Nape aliwataja kuwa ni mzigo kwa chama cho.

Katika mkutano wa hadhara wilayani Namtumbo, Ruvuma, Novemba 18 mwaka huu, Nape aliwataja baadhi ya mawaziri kuwa mzigo kwa chama cha na kutaka waitwa mbele ya Kamati Kuu kuhojiwa.

Mawaziri hao ni pamoja na Dk. Shukuru Kawambwa, akituhumiwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi Progressive ambayo ilishindwa kazi ya kujenga barabara ya Namtumbo hadi Tunduru; Chiza na Malima kwa kushindwa kutatua kero za wakulima wa korosho nchini.



Kwa ufafanuzi huu, tunamuomba radhi Profesa Maghembe kwa habari tulioandika kuhusu mawaziri ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao, na kwa vyovyote vile hatukuwa na nia ya kumchafua bali kutoa taarifa kwa umma kwa yale ambayo yanaelezwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali juu ya uwajibikaji katika ofisi za umma.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: