BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SPECIAL PHOTOS: MANISPAA YA MOROGORO DESEMBA 22/ 2013.





DESEMBA 21:Wateja wa benki ya nbc Manispaa ya Morogoro wakiwa kwenye foleni ndefu ya kuchukua fedha katika mashine za ATM makao ya benki hiyo baada ya baadhi ya mashine za beki hiyo kukumbwa na hitilafu za kiufundi na kuleta usumbufu kwa wateja wake mkoani Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG

DESEMBA 21:Kijana mkazi wa Manispaa ya Morogoro akiwa amebeba madumu tupu wakati akisaka kituo chenye mafuta kwa ajili kuendeshea mitambo na matumizi mengi baada ya kupewa kazi hiyo na mwaajili wake ambako wakazi wa maeneo ya vijijini wamekuwa wakitumia nishati hiyo katika matumizi ya mashine za kusaga nafaka na koroboi kwa ajili ya kupata mwanga katika nyumbani zao kutokana na sehemu kubwa kukosa huduma ya umeme mkoani Morogoro.PHOTO/MTANDA BLOG

DESEMBA 11:Treni ya abiria likiwa limekwama katika stesheni ya Morogoro kwa abiria kukaa kwa zaidi ya saa moja kufuatia treni hiyo kushindwa kuendelea na safari kulikotokana na treni hiyo kushindwa kupandisha kilima cha Kwamnyonge mara tatu mkoani Morogoro.PHOTOS/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: