BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJUMBE WA SIMU YA MKONONI ALIOKUSUDIA KUTUMWA KWA HAWALA BADALA YAKE WAENDA KWA MUME WA NDOA, TUKIO LAFANYWA NA ASKARI WA KIKE NA KUAMUA KUJIUA KUKWEPA FEDHEHA NA AIBU.


Mwanamke huyu aitwae Gail Crocker ambae alikua Polisi nchini Uingereza imefahamika kwamba alijiua baada ya kumtumia mume wake meseji badala ya kumtumia mpenzi wake ambae alikua polisi mwenzake.


Kwenye msg yenyewe, Gail aliandika kumshukuru mpenzi wake kwamba aliinjoy walipotoka pamoja usiku mmoja, na kumwambia ‘natamani tungekua tunafanya hivi mara kwa mara’.


Taarifa imesema Askari huyu ambae ni mama wa watoto wawili alikua akishiriki kwenye penzi la nje na askari mwenzake wakati mumewe akiwa kwenye safari za kibiashara ambapo baada ya kukosea msg aliamua kujiua kwa kunywa vidonge vingi na kujilaza kwenye buti ya gari.


Hata hivyo pamoja na Mwanamke huyo kutoka nje ya ndoa, mume wake ambae wamekua kwenye ndoa kwa miaka 30, Peter Crocker mwenye miaka 49, amesema Gail alikua Mwanamke wake wa maisha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: