BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANACHAMA WA KLABU YA SIMBA SC WAMSHURUTISHA MWENYEKITI WAO ISMAL ADEN RAGE KUJIULU KWA HIYARI KESHO JUMAMOSI, VINGINEVYO WANACHAMA WATAANDAA MAANDAMANO HADI KWA SPIKA WA BUNGE KUMSHTAKI MJINI DODOMA.

http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/Ismail%20Aden%20Rage(1).jpgDAR ES SALAAM.
WANACHAMA wa Simba wamemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage kujiuzulu hadi ifikapo Jumamosi la sivyo wataandamana kwenda bungeni mjini Dodoma.


Wanachama hao wakiwakilishwa na wenyeviti wao wa matawi Mkoa wa Dar es Salaam walisema jana, lengo la maandamano hayo ni kumshtaki Mwenyekiti huyo kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa kitendo chake cha kusigina katiba ya klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi.

Masoud Hassan ‘Ustadhi’ mwenye kadi namba 536 ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa alisema: “Tunataka mkutano, wanachama ndio wenye uamuzi wa mwisho, Rage ajiuzulu tunampa mpaka Jumamosi la sivyo Jumatatu tunamzukia bungeni, jimbo lake la Tabora Mjini analoliwakilisha si kubwa kama Klabu ya Simba.

“Kwanza amekiuka katiba yetu ibara ya 22 inayozungumzia mkutano wa dharura, unaotakiwa kuitishwa ndani ya majuma mawili yani siku 14 licha ya TFF kumheshimu na kutangaza kumtambua na wakamtaka aitishe mkutano pia amekaidi, sasa huko bungeni anakotunga sheria, anatunga sheria gani ambazo anazivunja tena kwa makusudi.

“Amekiuka pia ibara ya 40 inayozungumzia chombo cha haki, mpaka leo hajaunda chombo kitakachosimamia masuala mbalimbali ya uamuzi ndani ya Simba, nafasi ya Makamu mwenyekiti Geofrey Nyange ilitakiwa ijazwe ndani ya siku 90 lakini mpaka leo haijajazwa.

“Kibaya zaidi amekiuka ibara ya 2 (2) kwa kumteua Michael Wambura kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji wakati Wambura alisimamishwa uanachama wa Simba Mei 5 mwaka 2010 yeye na Juma Ntema baada ya kwenda mahakamani na hatma yao ilikuwa iamuliwe na mkutano mkuu wa wanachama ama kusamehewa adhabu yao na kurudishwa kundini au kuvuliwa uanachama,” alidai.

Kutokana na hali hiyo, Ustadhi alisema licha ya kumtaka Rage ajiuzulu kwa hiyari pia hatma yake itajulikana kwenye mkutano mkuu wa dharura wa wanachama kwa kumchukulia adhabu zaidi Mwenyekiti huyo kwa kukiuka katiba yao.

Hata hivyo, Wambura alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema, “Walichoongea ni mawazo yao na hiyo barua ya mimi kufungiwa Simba kama wanayo ni ya kwao hao mimi sijawahi kuiona.”

“Isitoshea kusuluhisha migogoro si lazima niwe mwanachama wa Simba, Rais Mkapa alipoenda kusuluhisha mgogoro Kenya kwani yeye ni Mkenya?” alihoji.


Simba imeingia kwenye mgogoro baada Kamati ya Utendaji chini ya Joseph Itang’are ‘Kinesi’ kumsimamisha Rage kwa kile walichodai ni kukiuka katiba.

Hata hivyo, Rage alipinga kwa kile alichodai kikao kilichomsimamisha ni sawa na kikao cha harusi.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema Kamati ya Utendaji ya TFF itakaa Desemba 22 kujadili iwapo Rage ataitisha mkutano wa wanachama alioagizwa na chombo hicho au hapana ambapo alipewa siku 14 hadi leo. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: