Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari moja
limelipuka mjini Maiduguri Kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuna hofu
ya watu wengi kujeruhiwa.
Majeruhi walionekana wakitoroka eneo la shambulizi ambalo lilikuwa na uharibifu mkubwa, huku wanajeshi wakifyatua risasi hewani.
Duru zinasema kuwa huenda shambulizi lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Habari zaidi zinakujia hivi punde.BBC

0 comments:
Post a Comment