Mkuu wa
Kituo cha Polisi Kimara (Mwenye shati la blue akijaribu kuzuia vijana
waliokuwa wanaiba Diesel kwenye gari iliyopata ajali
Kufa kufaana? Vijana waliingia kazini na kuanza kuchota mafuta baada ya kuokoa majeruhi..
Ajali mbaya
ya gari aina ya Lori imetokea leo mchana majira ya saa 7 maeneo ya
Kimara. Chanzo cha habari toka eneo la tukio kimesema ajali hii
imetokea baada ya Dereva wa Lori kuwa kwenye mwendo kasi na kushindwa
kuhimili breki za gari yake baada ya kukutana na kona ya gafla katika
ya vizuizi vya magari yaendayo kasi katika barabara hiyo inayoendelea
na ujenzi.
ChingaOne
blog ilifanya mahojiano na baadhi ya watu katika eneo la tukio na
kugundua kuwa wananchi wengi wamechoshwa na ujenzi wa bararaba hiyo
iliyochukua muda mrefu ambayo kwa sasa imekuwa kero kwa watuaji na mara
nyingi baadhi ya sehemu hufungwa na kufungulia bila taarifa kiasi cha
kuleta foleni na kusababisha ajali .
Baadhi ya
Wananchi wa Kimara wamesema kuna haja ya Serikali kuangalia muda wa
Ujenzi wa barabara hiyo inayotumika na wengi ikiwemo magari yanayofanya
safari ndani na nje ya nchi, Wameomba kuhamishiwa muda wa usiku ambapo
barabara inakuwa kimya na haitumiki na watu wengi ukilinganisha na muda
wa mchana.
Hadi
naandika habari hii kuna watu wawili wameng'ang'ania chini ya gari na
bado hayajatolewa hadi sasa ila cha ajabu kundi la Vijana limevamia eneo
hilo na kuanza kuiba mafuta yaliyokuwa kwenye gari lililopata ajali.http://www.chingaone.com
Endelea kuungana nasi kwa habari zaidi......

0 comments:
Post a Comment