BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO HII NI MBINU SAHIHI YA KUISHI.

 
KAMA una vidonda vya tumbo, matibabu yako yatategemea sababu ya vidonda vya tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama ni Non-Steroidal Anti-Inflamantory Drugs 'NSAIDS' mfano Aspirin & Ibuprofen utapaswa kutumia Proton Pump Inhibitor
'PPI' mfano Omeprazole & Esomeprazole. Ingawa matibabu ya siku hizi husisitiza kuchanganya dawa za kuua bakteria na Proton Pump Inihibitors 'PPI'.


Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri ukiwa na 'Vidonda Vya Tumbo':-
1. Acha kutumia kahawa na chai, kwa maana vitu hivi huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa na tumbo lako. Unaweza tumia chai ya mitishamba 'Herbal tea' kama mbadala.

2. Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na maziwa kama maziwa mgando 'Yoghurt', jibini 'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika
utumbo na kupunguza athari za asidi ya tumboni.

3. Jitahidi kupunguza uzito kama uzito umezidi na hauendani na kimo chako.


4. Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.


5. Acha au kunywa vileo siku maalumu tu kwa maana unywaji wa pombe mara kwa mara hutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

6. Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.


7. Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone. http://manyandahealthy.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: