Kocha mpya wa Yanga, Hans Van Der Pluijm.
Van Der Pluijm alisaini mkataba huo mbele ya
viongozi wa Yanga jana Jumatatu saa nane mchana katika ofisi za
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji zilizopo jengo la Quality Plaza, jijini
Dar es Salaam.
Kocha huyo aliwaambia viongozi wa klabu hiyo kuwa
anamfahamu vizuri kocha wa Simba, Zdravko Logarusic, kuanzia falsafa
yake na mbinu zake anazotumia uwanjani, hivyo ana uwezo mkubwa wa
kumshinda uwanjani.
Mdachi huyo aliwataka viongozi wa Yanga kutokuwa
na hofu yoyote juu yake na kuanzia sasa wanaweza kutembea kifua mbele
kwa kuwa hawatakuwa na hofu ya matokeo katika mechi zinazokuja mbele
yao.
Akizungumza na Mwanaspoti katika mahojiano
maalumu, Van Der Pluijm, alisema rekodi yake nzuri ni ile aliyomfunga
Logarusic mabao 4-1 wakiwa nchini Ghana wakati akiifundisha Berekum
Chelsea na mwenzake alikuwa akiinoa Ashanti Gold.
“Namfahamu vizuri kocha (Logarusic), ni kweli
nilimfunga mara ya mwisho tulipokutana, lakini sitaki kutumia matokeo
hayo na kuyaleta Yanga, mpira unabadilika lakini kwa kuwa namjua mbinu
zake, hawezi kunisumbua. Yanga wasiwe na wasiwasi ngoja nikatengeneze
timu,” Van Der Pluijm.
Akubali majukumu
Van Der Pluijm alikiri kupewa mikakati na uongozi namna ya kuiweka Yanga katika ramani ya soka Afrika ikiwamo
kuifikisha katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo
atatumia uzoefu wake ili kuhakikisha anafanikiwa.
“Nitatumia uzoefu wangu katika soka la Afrika
kutimiza matakwa ya Yanga, haya ni makubaliano yangu na uongozi.
Nimeshaanza kazi rasmi ndiyo maana nakueleza hata wewe mambo haya,
nimekuwa kwa muda mrefu katika kazi hii hapa Afrika. Nataka kutumia
uzoefu wangu kuipa mafanikio Yanga,” alisema Van Der Pluijm.
Aweka masharti
Akizungumzia aina ya soka analotaka Yanga, Van Der
Pluijm alisema anataka kuona kikosi chake kinacheza soka lenye asili ya
nchi tatu zikiwemo Brazil, Uholanzi na England. MWANASPOT

0 comments:
Post a Comment