MWANAMKE WA MTU AFANYA USALITI NDANI YA NDOA NI BAADA YA MUMEWE KUANZA KUMSALITI MKEWE NA KUGAWA URODA NJE YA NDOA NA KUMPACHIKA UJAUZITO MFANYAKAZI WAO WA NDANI..
PICHA YA MWANAMKE HAIUSIANI NA HABARI HII.
MIMI nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe.
Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe..
Wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu.
Kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
Sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..
Nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
Nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote.
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona kama nazidiwa mawazo vile.
HUYU NDIYE MKE WA MTU ALIYEAMUWA KUGAWA URODA NJE YA NDOA KISA MUMEWE KAZIDI USALITI....SASA ANAOMBA USHAURI - SKY BONGO
Pole saana kwa mambo mazito yaliyopo kwenye familia yenu. Swala lenu ni zito saana! Manake Mume kamwaga mboga na mama akaamua kumwaga ugali!
Mtihani wa kuutakasa ugali na mboga vifae kulika bila uchafu ni swala tete saana! Kwa kweli pa kuanzia ni kuamua kutengana kama mmoja wenu hajaathirika na virusi.
Halafu swala la nyumba linaweza kutatuliwa mkishapeana talaka. Pia inaonekana sasa hakuna upendo tena wa kweli kwenye ndo yenu !
Kifupi hakuna tena baraka za Mungu katika hayo mnayofanya! Yeye kama kampenda HG na kaamua kubobea huko akupe talaka yako! Wewe pia ujasema huyo anayekuliwaza ni Mume wa mtu ama Mme mtarajiwa!
Kama ni mume wa mtu basi itabidi pia ujipage kupata mume wako wa halali manake utakapotoka kwa huyo ukaendelea kuhudumiwa na mume wa mtu bado utakuwa huna baraka wala amani na furaha ya uhakika !
Pia utambue kwamba kufanya kosa la kutembea nje ya ndoa siyo jawabu la mume wako kutembea na HG wako hata akampa mimba! Yamkini wakati akitembea na huyo HG pengine ulikuwa pia una matatizo fulani ama ya uzazi ama matatizo mengineyo.
Bahati mbaya pia kuna mengi yamejificha hapo ukuyaweka wazi! Kwa mfano alipokucheat mwanzo akiwa nje ya nchi ukusema alibainisha ni sababu gani zilimfanya ashindwe kujiheshimu na kufanya kosa hilo.
Pia wakati walianza mahusiano na HG ingekuwa vyema kujua kwa nini alishawishika kucheat! Kimsingi kama mlianza na Mungu katika ndoa yenu basi inabidi mfanye jitihada maksudi kabisa kumtafuta tena na kujitenga na shetani!
Kimtizamo ww unaweza kudhani kutembea nje ndiyo kumkomoa mume wako kumbe bado dawa ya kosa si kufanya tena kosa! Ungepaswa kuendelea kuwa mwamiifu na hakika unastahili kuendelea kuwa mwaminifu na kutegemea huruma ya Mungu kurudi kwenye nafasi yako! Mume wako pia tungepata fursa ya kusikia ya kwake tungeweza kumshauri yeye afanye nini !
Poleni saana lakini bado mnatakiwa kuchukua hatua kurekebisha maisha yenu ili jambo baya zaidi lisitokee kwa sasa mkiwa mnaishi bado nyumba moja wakati kiukweli hamna tena upendo katika ndoa yenu!!
0 comments:
Post a Comment