Steve Mangere ‘Steve Nyerere’.
NDANI ya klabu ya mastaa wa sinema za
Kibongo, Bongo Movie Unity (au Bongo Muvi), kumetibuka upya baada ya
mwenyekiti na kiongozi mpya wa kundi hilo, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ kuanika makubwa na mazito juu ya uchafu, ufuska na mtandao
nzima wa ‘kushea’ wapenzi miongoni mwao, aya zinazofuata zitakupa
mwanga.
Akiwa amezungukwa na jopo la wahariri wa
Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar hivi karibuni,
kwa utulivu wa hali ya juu, Steve Nyerere alifunguka mengi.
Katika intavyu hiyo, maswali yaliulizwa
kwa mtindo wa kupokezana na umakini wa hali ya juu ambapo ‘komediani’
huyo aliweka bayana jinsi ambavyo wasanii wamekuwa wakibadilishana
wapenzi kama siti za daladala huku ugomvi, majungu na unafiki
vikichochewa na tabia hiyo.
Bila kuonesha woga wala wasiwasi,
mwenyekiti huyo alikiri kuwa wasanii wengi wenye majina makubwa ndani na
nje ya Bongo Muvi, ndiyo vinara na wafuasi wakubwa wa mtandao huo
mchafu wa ngono.
Aliongeza kuwa, ilifika wakati klabu hiyo ikawa inatafsiriwa kama uwanja wa kugawana wapenzi kama mbegu za mahindi.
AWATAJA VINARA
Kwa sauti ya kuumiza masikio, Steve aliwataja kwa majina baadhi ya wasanii hao (ukitaka kuwajua, njoo ofisini tukutajie).
MIGONGANO
Alisema kuwa wapo ambao kwa namna moja
au nyingine wamesababisha migogoro na migongano mikubwa ndani ya klabu
hiyo kufuatia vitendo hivyo vya kuchangia wapenzi kama wafanyavyo
wanyama ndani ya mbuga za Serengeti, Mikumi na nyinginezo.
“Ni kweli kabisa vitendo vya ngono, kubadilishana na kuchangia wapenzi vimekithiri Bongo Muvi.
“Utakuta msanii huyu wa kiume anatoka
kimapenzi na msanii yule wa kike, lakini wasanii wengine nao bado
watataka kumchukua mmoja wao. Au msanii yuko katika uhusiano na msanii
mwenzake, lakini anaanzisha uhusiano na mwingine bila kujali kuwa huyo
naye ana mwingine na anamjua.
“Mzunguko unakuwa mkubwa na wanaoongoza kwa ufuska huo ni hawa wasanii ambao wanaonekana mastaa.
MFANO
“Kwa mfano, wasanii kama (akawataja
majina) walikuwa na ‘cheni’ hii ya wapenzi, ...(akamtaja jina) alikuwa
na uhusiano na ...(akimtaja shori mkali wa sinema za Kibongo), wakati
huohuo,... (akamtaja staa mwingine jina) ana uhusino na msanii ambaye
alikuwa kuwa na.... (akawataja kwa majina), sasa unaona jinsi ambavyo
mzunguko unakuwa wa hatari zaidi,” alisema Steve Nyerere.
AMELALA NA WANGAPI ?
Bila kutegemea, msanii huyo aliulizwa na
kutakiwa ataje wasanii ambao aliwahi ‘kudondoka nao kunako sita kwa
sita’ ambapo alishikilia msimamo kuwa hajawahi kwa sababu ambazo
alizitaja kwa hisia kali.
Jamaa huyo aliweka angalizo kuwa si
rahisi kwa mtu kuamini kuwa yeye hajawahi kucheza mchezo wa ‘baba na
mama’ na msanii yeyote ndani ya kundi hilo.
KIBAO CHAMGEUKIA
Baada ya kuachana na upande wa wasanii,
kibao kilimgeukia yeye ambapo wahariri walianza kumtandika maswali
magumu na makali yaliyomlenga yeye tu kama ifuatavyo:
Swali: Vipi skendo ya wewe kuwakuwadia wasanii wa kike kwa vigogo?
Steve: (akikunja ndita) hapana jamani,
hayo ni maneno tu, mwanzoni watu wengi walidhani hivyo, lakini mimi
niliwavuta vigogo ndani ya klabu kwa lengo la hisani na udhamini,
namshukuru Mungu baadaye walinielewa, lakini vigogo wote walijitoa kwa
sababu ya maneno kama hayo.
Swali: Bifu lako na Ray (Vincent Kigosi) na JB (Jacob Steven) lilikuwaje?
Steve: Ni mambo ya kazi tu, si unajua
binadamu tuna mapungufu, tulijikuta katika tofauti za kibinadamu, lakini
kwa sasa mambo yako sawa.
Swali: Vipi madai ya kwamba una ‘ngoma’?
Steve: (akitabasamu) jamani, mimi
nimepitia misukosuko mingi, lakini nimeendelea kushikilia nafasi yangu
ya usanii. Ni kweli walizusha lakini ukweli ukabaki kuwa niko salama.
“Lakini si jambo geni kwa mtu kuzushiwa
ugonjwa huo, hata ninyi (wahiriri) mnaweza kusingiziwa mambo mengi na
maadui wenu kwa hiyo ni uzushi, niko fiti na tayari kwa mapambano.”
Swali: Eti wewe ni mtu wa ushirikina sana?
Steve: Duh! Si kweli jamani, nimezaliwa
na kukulia kwenye familia ya Kikristo, namwamini Mungu kuliko kitu
kingine chochote, siwezi kufanya hivyo.
Swali: Ilidaiwa ulimuua mwanao kwa kumtoa kafara, hili likoje?
Steve: (utulivu kidogo, anakuna kichwa)
hakuna kitu kama hicho, kama nilivyosema hapo awali mimi ni Mkristo,
mambo ya riziki hupangwa na Mungu, sasa nimtoe mwanangu kafara kweli?
Siwezi jamani, siyo kweli.
KUTOKA RISASI
Wasanii ni kioo cha jamii, ni vyema kama
wataishi maisha ya kuigwa na jamii huku wakijikita zaidi katika
uboreshaji wa kazi zao na kuitangaza sanaa yetu kimataifa zaidi-
Mhariri.
0 comments:
Post a Comment