Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Ndugu Bernard Membe
akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa NEC mara baada ya
kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ambapo alisema Kamati ya Maadili
imeuliza masuala mazito na maswali magumu yanayohusiana na uvunjaji wa
maadili ya uongozi wa chama. BAADA ya kuhojiwa na kamati ndogo ya maadili ya CCM mjini dodoma, Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amesema kwamba licha ya kuwa na yeye amewekwa kitimoto na kamati hiyo ambayo inashughulikia wanaojinadi kugombea urais kabla ya wakati, anaipongeza kamati hiyo na anaungana nayo kwa asilimia mia moja.
Bwana Membe amesema haitakuawa busara kuacha watu waendelee kujinadi kabla ya wakati na huku wengine wakijaribu kununua uongozi wa nchi. "huwezi ukanunua uongozi, naungana na kamati katika hili, acha chama kiamue nani anafaa na nani hafai" alisema Bw. Membe.
Membe amekaririwa pia akiwaasa waandishi wa habari kuacha kuchagua habari za kuandika kwa kuangalia uwezo na sura za watu ila wawe wakiandika habari zote za msingi bila kuwanyima watanzania haki yao ya kupata habari kwa mambo yote yanayoendelea ndani ya nchi yao.

0 comments:
Post a Comment