BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HUYU NDIYE MBUNGE WA KWANZA WA CCM KUWEKA HISTORIA YA KUTOLEWA NJE YA KIKAO CHA BUNGENI, JE WAMFAHAMU NA KWANINI ALITOLEWA ?.


“Katika kikao hicho tuliangalia mambo makuu ambayo yanaziwezesha hizi sehemu mbili kujitegemea ikiwamo ofisi muhimu kama vile: matawi ya benki mbalimbali, Tanesco, Ofisi ya Mamlaka ya Mapato na vituo vya Polisi,” Dk. Ndungulile.
Ni miongoni mwa wabunge wanaowakilisha majimbo yao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Moja ya sifa ya kipekee aliyonayo ni kuwa na Jimbo lenye wakazi wengi kuliko majimbo mengine, lina wakazi wapatao 750,000, na ni moja ya Jimbo lenye changamoto nyingi ikiwemo ujenzi wa Mji Mpya wa kisasa wa Kigamboni.

 Dk. Ndungulile akisisitiza jambo

Huyu si mwingine bali ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile, ambaye alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na mwandishi wa gazeti hili, akieleza ushiriki wake katika siasa.


Asichokisahau katika kipindi cha miaka minne aliyokuwa bungeni ?.
Ndungulile anasema, hatoweza kusahau siku ambayo aliandika historia ya kuwa mbunge wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi, kutolewa bungeni akitetea haki za wananchi wa jimbo lake.


“Siwezi kulisahau hilo kwa mawili; kwanza nilikuwa natetea wananchi wangu, najivunia kuwa kama ni kifo ningekufa shujaa, lakini pili ni kuwa mbunge wa kwanza kutoka CCM, kutolewa nje ya Bunge, haikuwa hali ya kawaida,” anasema.


“Sitaki kulizungumzia kwa undani hilo kwa kuwa lilikwishapita lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali adhabu ya Naibu Spika Job Ndugai ya kutoka nje ya Bunge kwa muda wa siku tatu kwa kuwa alitumia kanuni ambayo imekuwa ikimlinda,” anasema Ndungulile.


Kanuni iliyomtoa
Anaitaja Kanuni aliyotumia Spika kumtoa nje ya kikao cha Bunge kuwa ni kanuni ya 73 (3) ambayo inasema:


Endapo mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha ukweli wa maneno aliyoyasema hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa na kukataa ama kushindwa kutoa uthibisho huo Spika anaweza kumsimamisha asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano.


Anasemaje kuhusu kuligawa Jimbo la Kigamboni?
Ndungulile anafafanua kuwa mwezi uliopita walikuwa na kikao na Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Temeke, azimio kuu likiwa ni kuligawa Jimbo la Kigamboni na kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi kwa maana ya Mbagala na Kigamboni.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: