BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS, WAZIRI MKUU HUENDA WAKAIPONZA TANZANIA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU YA BINADAMU (ICC).


MKURUGENZI WA KITUO HIKO DEUS KIBAMBA AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI

Na Karoli Vinsent
KAULI aliyopata kuitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni kuwataka polisi wawapige wapinzani, na kauli ya juzi ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo pale wanaposhambuliwa na wapinzani, imeelezwa kuliingiza taifa vitani. Kituo Cha taarifa kwa Wananchi (TCIB) kimeanza mawasiliano na Mwendesha Mastaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uharifu dhidi ya Binadamu (ICC) Bi Fatou Bensouda kumwomba atume timu ya wataalamu wake kuja Tanzania kufanyia Uchunguzi na Tathmini kuhusu kauli hizo iliwaweze kuifungulia mashtaka Serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi wa Kituo
Cha taarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari alisema kuwa wameamua kufanya Maamuzi hayo kwa kuona Amani ya nchi inaanza kutoweka kutokana na viongozi kutoa matamshi yanayochochoe uvunjifu wa amani.


“Tumeamua kuchukua hatua hii kufanya mawasiliano na Mwendesha Mastaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uharifu dhidi ya Binadamu(ICC) Bi Fatou Bensouda baada ya kuwa na hofu kuwa tukiachi matamshi”

“ haya yaendelee, kunaweza kutokea fujo kubwa na kupelekea mauaji ya ajabu huko tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,leo kiongozi mkubwa kama Rais anatoa kauli hizi tena mbaya,hivi anafikiria wakati anatoa kauli hizi,leo anafikiri amani hii ikivunjika yeye nani atabaki hapa”alisema Kibamba

Kibamba ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Nchini alisema Taifa la Tanzania litaingia kwenye machafuko kwani nchi ya Jirani ya Kenya dalili zake zilikuwa kama za Tanzania.

“Mimi kwenye uchaguzi wa Kenya wa Mwaka 2007 nilikuwepo na Dalili za machafuko zilitokana na viongozi kama hawa kutoa kauli za kukashifu na katoa amasa kwa wananchi kulipiza kisasi,leo hawo greengurd wakishambulia redgurd au redgurd wakiwashambulia Greengurd kunamtu atapona,manaake amani ya nchi ndio inavunjika hapo”alisema Kibamba.

Ikumbukwe tamko la Kibamba limekuja kutokana na kauli ya Rais kikwete, wakati Akifungua mkutano wa NEC ya CCM juzi mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.

Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.

“Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.

Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

“Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake,” alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.

“Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,” alisema.

Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.
CHANZO http://habari24.blogspot.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: